Pata taarifa kuu

Rwanda yajiandaa kuadhimisha miaka thelathini ya mauaji ya kimbari ya Watutsi

Rwanda inaadhimisha leo Jumapili kumbukumbu ya miaka 30 ya mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994 ambapo Wahutu wenye msimamo mkali waliwaua watu karibu milioni moja wengi wao wakiwa ni Watutsi.

Muonekano wa mlango wa ukumbusho wa mauaji ya Bisesero yaliyofanywa wakati wa mauaji ya Watutsi nchini Rwanda, Desemba 2, 2020.
Muonekano wa mlango wa ukumbusho wa mauaji ya Bisesero yaliyofanywa wakati wa mauaji ya Watutsi nchini Rwanda, Desemba 2, 2020. © SIMON WOHLFAHRT/AFP
Matangazo ya kibiashara

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza April 7 mwaka 1994 na vilivyodumu kwa siku 100, vilishuhudiwa siku moja tu baada ya kudunguliwa kwa ndege aliyokuwamo rais wa wakati huyo wa Rwanda Juvénal Habyarimana pamoja na yule wa Burundi Cyprien Ntaryamira.

Viongozi hao walikuwa wametoka kwenye mkutano wa kilele nchini Tanzania ambako walikuwa wanajadili mzozo huo wa Rwanda. Mauji ya kimbari ya mwaka 1994 ni miongoni mwa matukio mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Rwanda.

Hadi leo hii, makaburi ya jumla yanaendelea kugundulika katika nchi hiyo yenye watu karibu milioni 14. Viongozi mbalimbali akiwemo aliyekuwa rais wa Marekani wakati wa mauaji hayo Bill Clinton wanatarajia kuhudhuria maadhimisho hayo.

Siku ya Alhamisi Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema kwamba Ufaransa na washirika wake wangeweza kukomesha mauaji ya halaiki lakini hawakuwa na nia ya kufanya hivyo. Tamko la Macron lilikuja miaka mitatu baada ya kukiri jukumu kubwa la Ufaransa mshirika wa karibu wa Rwanda wa Ulaya mwaka 1994 kwa kushindwa kuzuia kuingia kwa nchi hiyo kwenye mauaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.