Pata taarifa kuu

Emmanuel Macron: Ufaransa na washirika wake haikuwa na nia ya kokomesha mauaji Rwanda

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anasema Ufaransa ambayo "ingeweza kukomesha mauaji ya halaiki na washirika wake wa Magharibi na Afrika, haikuwa na nia" kulingana na ikulu ya Ikulu ya Élysée.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akitoa hotuba pamoja na Kansela wa Austria wakati wa mkutano na waandishi wa habari kabla ya chakula cha mchana katika ukumbi wa Elysée mjini Paris, Aprili 4, 2024.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akitoa hotuba pamoja na Kansela wa Austria wakati wa mkutano na waandishi wa habari kabla ya chakula cha mchana katika ukumbi wa Elysée mjini Paris, Aprili 4, 2024. AFP - MOHAMMED BADRA
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Rais Emmanuel Macron, Ufaransa ambayo "ingeweza kukomesha mauaji ya kimbari na washirika wake wa Magharibi na Afrika, haikuwa na nia", iliripoti Élysée siku ya Alhamisi, wakati Rwanda inajiandaa kuadhimisha kwa siku 100 miaka 30 ya mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi. Mauaji yaliyoanza Aprili 7, 1994 na kusababisha vifo kati ya watu 800,000 na milioni moja.

Rais wa Ufaransa, ambaye alitambua mnamo 2021 "wajibu" wa nchi yake katika mauaji ya kimbari, atazungumza Jumapili "kupitia video ambayo itarushwa kwenye mitandao yake ya kijamii", kimeongeza chanzo katika Ikulu ya Élysée.

"Mkuu wa Nchi atakumbusha haswa kwamba, wakati awamu ya kuwaangamiza kabisa Watutsi ilipoanza, jumuiya ya kimataifa ilikuwa na njia ya kujua na kuchukua hatua, kupitia ujuzi wake wa mauaji ya halaiki yaliyofichuliwa kwetu na manusura wa Waarmenia na Shoah, na kwamba Ufaransa, ambayo ingeweza kukomesha mauaji ya halaiki pamoja na washirika wake wa Magharibi na Afrika, haikuwa na nia ya kufanya hivyo,” kinabainisha chanzo hicho.

Akialikwa kwenye maadhimisho hayo na Rais wa Rwanda Paul Kagame, Emmanuel Macron hatahudhuria. Atawakilishwa katika maadhimisho hayo na Waziri wa Mambo ya Nje, Stéphane Séjourné, na Katibu Kiongozi anayehusika na msuala ya Bahari, Hervé Berville, ambaye alizaliwa nchini Rwanda Januari 15, 1990.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.