Pata taarifa kuu

Rwanda kuadhimisha Jumapili miaka 30 ya mauaji ya kimbari

Rwanda inajiandaa kuadhimisha siku ya Jumapili kumbukumbu ya miaka 30 ya mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994 ambapo Wahutu wenye msimamo mkali waliwaua watu karibu milioni moja wengi wao wakiwa ni Watutsi.

Mafuvu ya vichwa na mifupa ya baadhi ya waliochinjwa walipokuwa wakitafuta hifadhi ndani ya kanisa hilo yamewekwa kama kumbukumbu ya maelfu ya watu waliouawa ndani na nje ya Kanisa Katoliki wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 huko Ntarama, Aprili 4, 2014. Mahakama ya Rwanda iliwatia hatiani viongozi kadhaa waliohusika katika mauaji ya halaiki ya taifa hilo la Afrika mwaka 1994 wakati takriban watu 800,000, hasa Watutsi waliuawa.
Mafuvu ya vichwa na mifupa ya baadhi ya waliochinjwa walipokuwa wakitafuta hifadhi ndani ya kanisa hilo yamewekwa kama kumbukumbu ya maelfu ya watu waliouawa ndani na nje ya Kanisa Katoliki wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 huko Ntarama, Aprili 4, 2014. Mahakama ya Rwanda iliwatia hatiani viongozi kadhaa waliohusika katika mauaji ya halaiki ya taifa hilo la Afrika mwaka 1994 wakati takriban watu 800,000, hasa Watutsi waliuawa. AP - Ben Curtis
Matangazo ya kibiashara

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza April 7 mwaka 1994 na vilivyodumu kwa siku 100, vilishuhudiwa siku moja tu baada ya kudunguliwa kwa ndege aliyokuwamo rais wa wakati huyo wa Rwanda Juvénal Habyarimana pamoja na yule wa Burundi Cyprien Ntaryamira.

Viongozi hao walikuwa wametoka kwenye mkutano wa kilele nchini Tanzania ambako walikuwa wanajadili mzozo huo wa Rwanda. Mauji ya kimbari ya mwaka 1994 ni miongoni mwa matukio mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Rwanda.

Hadi leo hii, makaburi ya jumla yanaendelea kugundulika katika nchi hiyo yenye watu karibu milioni 14. Viongozi mbalimbali akiwemo aliyekuwa rais wa Marekani wakati wa mauaji hayo Bill Clinton wanatarajia kuhudhuria maadhimisho hayo.

Siku ya Alhamisi Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema kwamba Ufaransa na washirika wake wangeweza kukomesha mauaji ya halaiki lakini hawakuwa na nia ya kufanya hivyo. Tamko la Macron lilikuja miaka mitatu baada ya kukiri jukumu kubwa la Ufaransa mshirika wa karibu wa Rwanda wa Ulaya mwaka 1994 kwa kushindwa kuzuia kuingia kwa nchi hiyo kwenye mauaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.