Pata taarifa kuu

Rwanda yaadhimisha mauaji ya kimbari ya Watutsi, miaka 30 baadaye

Miongo mitatu ya ujenzi upya: Rwanda inaadhimisha tangu Jumapili mauaji ya halaiki ya Watutsi, siku 100 za huzuni ambapo kiza bado kinatanda katika nchi hii ya Maziwa Makuu ya Afrika, licha ya kazi ya maridhiano isiyo na mwisho.

Wanakijiji na watu wa kujitolea wakichimba mabaki ya wahanga wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 yaliyofichwa chini ya msingi wa nyumba huko Ngoma, Rwanda, Januari 23, 2024, ambapo zaidi ya miili 82 imepatikana tangu Januari 21 2024.
Wanakijiji na watu wa kujitolea wakichimba mabaki ya wahanga wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 yaliyofichwa chini ya msingi wa nyumba huko Ngoma, Rwanda, Januari 23, 2024, ambapo zaidi ya miili 82 imepatikana tangu Januari 21 2024. AFP - GUILLEM SARTORIO
Matangazo ya kibiashara

Sherehe rasmi zitaanza Aprili 7 - siku ya mauaji ya kwanza ya kile kilichokuwa mauaji ya mwisho ya halaiki katika karne ya 20, na kusababisha vifo vya watu 800,000, haswa miongoni mwa Watutsi walio wachache, lakini pia Wahutu wenye msimamo wa wastani.

Kama kila mwaka, Rais Paul Kagame - kiongozi wa Rwandan Patriotic Front (RPF) ambaye alipindua utawala wa Kihutu wa mauaji ya halaiki mnamo mwezi Julai 1994 na amekuwa shujaa wa nchi hiyo tangu wakati huo - atawasha mwali wa ukumbusho kwenye Kumbukumbu ya Gisozi mjini Kigali.

Sherehe hii, mbele ya viongozi wa serikali na viongozi wa kigeni, itaashiria kuanza kwa wiki ya heshima, ambayo itashuhudia shughuli nyingi zikipungua nchini. Muziki hautaruhusiwa katika maeneo ya umma au kwenye redio. Matukio ya michezo na filamu zitapigwa marufuku kutangazwa kwenye televisheni, isipokuwa kama zimeunganishwa na ukumbusho.

“Mende”

Mauaji ya majira ya kuchipua 1994 yalichochewa siku moja baada ya shambulio la ndege ya rais wa Kihutu Juvénal Habyarimana, katika hali ya chuki iliyochochewa na propaganda mbaya dhidi ya Watutsi.

Kwa muda wa miezi mitatu, jeshi, wanamgambo wa Interahamwe na pia raia wa kawaida waliwaua kwa bunduki, mapanga au marungu - Watutsi, walioitwa "Inyenzi" ("mende" kwa lugha ya Kinyarwanda), lakini pia wapinzani wa Kihutu. Mauaji hayo yaliisha wakati waasi wa Watutsi wa RPF walipoteka Kigali mnamo Julai 4, na kusababisha mamia ya maelfu ya Wahutu walio kuwa na hofu kuhama kwenda Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo).

Miaka 30 baadaye, makaburi ya halaiki yanaendelea kufukuliwa. "Mwaka huu, tunakumbuka mzizi mbaya wa mauaji ya halaiki: chuki," amesema Antonio Guterres, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa. "Kwa wale wanaotaka kutugawa, lazima tutoe ujumbe wazi, usio na shaka na wa dharura: kamwe tena." Jumuiya ya kimataifa ilikosolewa vikali kwa kutochukua hatua, na Umoja wa Mataifa kwa kuondoa vikosi vyake baada ya ghasia za kwanza.

"Nguvu tofauti"

Kwa miaka 30, Rwanda imekuwa ikifanya kazi ya upatanisho, hasa kwa kuundwa mwaka 2002 kwa mahakama za kijamii, "gacaca" ambapo waathiriwa wanaweza kusikiliza "maungamo" ya wauaji.

Kadi za utambulisho hazitaji tena ukabila, na historia ya mauaji ya halaiki inafunzwa katika mtaala unaodhibitiwa vilivyo. Leo, zaidi ya 70% ya watu milioni 13 wa Rwanda wana umri wa miaka 30 au chini. Bila kusahau yaliyopita, wanakusudia kujikomboa kutoka katika uzito wa mauaji ya kimbari ambayo hawakushuhudia.

"Tangu nikiwa mdogo, historia ya Rwanda imekuwa ya ujenzi upya," Roxanne Mudenge, meneja wa mradi wa umri wa miaka 27, anaelezea shirika la habari la AFP: "Makovu ya siku za nyuma bado yapo, lakini sasa kuna nguvu tofauti, hisia ya uwezekano."

Vyombo vya sheria pia vilichukua jukumu kubwa lakini kulingana na Kigali, mamia ya watu wanaoshukiwa kushiriki katika mauaji ya halaiki bado wako huru, haswa katika nchi jirani, kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Uganda.

Jumla ya watoro 28 wamerejeshwa kutoka mataifa ya kigeni wakiwemo sita kutoka Marekani. Ufaransa haijamrudisha hata mmoja wao lakini imewahukumu nusu dazeni. Paris, ambayo ilidumisha uhusiano wa karibu na utawala wa Kihutu wakati mauaji ya halaiki yalipoanza, kwa muda mrefu imekuwa ikishutumiwa kwa "ushirikiano" na Kigali.

Tume ya wanahistoria iliyoundwa na Emmanuel Macron ilihitimisha mnamo mwaka 2021 kwamba Ufaransa ilikuwa na "majukumu mazito na mabaya", huku ikifutilia mbali kuhusika wala kushiriki. Ripoti hii iliruhusu maelewano ambayo hayajawahi kutokea, baada ya miongo kadhaa ya mivutano.

Mivutano ya kidiplomasia

Hata hivyo, uhusiano haujatulia na DRC ambayo, kulingana na ofisi ya mwendesha mashtaka wa Rwanda, inahifadhi idadi kubwa ya washukiwa waliokimbia (408). Shutuma za pande zote za uvunjifu wa amani zimekuwa za mara kwa mara tangu kumalizika kwa mauaji ya kimbari. R PF ilishutumiwa kwa kuua makumi ya maelfu ya watu nchini Zaire (DRC sasa) katika kuwasaka wahusika wa mauaji ya halaiki.

Mvutano umeongezeka kwa kasi tangu mashambulizi ya M23, waasi wengi wao kutoka jamii ya Watutsi, mwishoni mwa mwaka 2021 mashariki mwa DRC. Kinshasa, pamoja na Umoja wa Mataifa, Marekani na nchi kadhaa za Magharibi zinaishutumu Kigali kwa kuwaunga mkono waasi hao. Kigali inakanusha kuhusika na inashutumu DRC kwa kuunga mkono kundi la Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR), kundi lenye Wahutu wengi lililoundwa na maafisa wakuu wa zamani wa mauaji ya halaiki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.