Pata taarifa kuu

Tanzania na Kenya kutatua mvutano wa safari za anga

Nairobi – Kenya na Tanzania zimekubaliana kutatua mvutano wa safari za anga ndani ya siku tatu zijazo, baada ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Tanzania kutangaza kusitisha safari za ndege za abiria za Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kwenda jijini Dar es salaam kuanzia Januari 22.

Hatua hii imekuja baada ya mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya nje wa Kenya Musalia Mudavadi na mwenzake wa Tanzania, Januari Makamba
Hatua hii imekuja baada ya mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya nje wa Kenya Musalia Mudavadi na mwenzake wa Tanzania, Januari Makamba REUTERS - Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya nje wa Kenya Musalia Mudavadi na mwenzake wa Tanzania, Januari Makamba.

Katika taarifa ya pamoja, iliyochapishwa kwenye kurasa zao za kijamii za X, Mawaziri hao wawili wamekuabaliana na kuapa kushughulikia changamoto zilizojitokeza, kwa nchi hizo mbili kutekeleza makubaliano ya ushirikiano wa safari za angaa.

Kabla habari hiyo, Tanzania ilikuwa imetangaza kusitisha safari za ndege za Kenya kwenda Dar es salaam, baada ya kuishtumu Kenya kwa kukataa ombi la Shirika la Ndege la Tanzania kuruhusu ndege ya mizigo ya Air Tanzania kusafirisha mizigo kutoka Nairobi kwenda mataifa mengine.

Mwaka 2020 nchi hizo mbili pia ziliingia kwenye mvutano kama huu, baada ya mamlaka za Tanzania kuzuia ndege za Kenya kutua nchini humo kwa madai  ya Nairobi, kuiwekea vikwazo vya kibiashara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.