Pata taarifa kuu

Tanzania: Watu 22 wamefariki katika mgodi wa dhahabu

Nairobi – Watu 22 wamefariki dunia baada ya kuporomoka kwa vifusi vya udongo katika mgodi wa dhahabu wa Ikinabushu wilayani Bariadi mkoa wa Simiyu nchini Tanzania

Ramani ya nchi ya Tanzania
Ramani ya nchi ya Tanzania © https://wwwnc.cdc.gov/
Matangazo ya kibiashara

Ajali hiyo imetokea Alfajiri ya kuamkia Jumamosi ya januari 13 wakati wachimbaji wadogo wa dhahabu wakiendelea zoezi la uchimbaji.

Hali ilikuwaje kabla ya kuporomoka mgodi huo, Steven Masumbuko ni msimamizi wa mgodi huo.

“Udongo ulikuwa umezidiwa ndio ukawaponda watu. ” alisema Steven Masumbuko.

00:10

Steven Masumbuko

Kaimu kamanda wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Faustine Mtitu amesema mpaka sasa miili yote imeokolewa.

“Zoezi letu la uhakiki limetuonyesha kwamba hakuna mtu aliyesalia kwenye mgodi huu. ” alieleza Faustine Mtitu.

00:15

Faustine Mtitu

Serikali imechukua hatua gani kufuatia ajali hiyo, Anthony Mavunde ni Waziri wa Madini nchini humu.

“Kabla hawajaendelea na hali ilivyo kwa sasa, kwa sababu hali ilivyo kwa sasa, madhara yanaweza kutokea tena. ” alieleza Anthony Mavunde.

00:15

Anthony Mavunde

Mgodi huo umeporomoka zikiwa ni takribani siku tatu tangu uanze kazi ya uchumbaji, ukiwa ni mgodi wa pili wa dhahabu kuporomoka katika kipindi cha miaka minne katika mkoa huo.

Steven Mumbi/ rfi Kiswahili/ Dar es salaam

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.