Pata taarifa kuu

Tanzania: Waliosambaza tuhuma kuhusu afya ya naibu rais kuchukuliwa hatua

Nairobi – Mamlaka nchini Tanzania zinawachunguza matumiaji wa mitandao ya kijami wanaotuhumiwa kwa kusambaza taarifa za uongo kuhusu afya ya naibu wa rais Philip Mpango.

Makamu wa rais wa Tanzania, Dr Philip Mpango.
Makamu wa rais wa Tanzania, Dr Philip Mpango. © TQA
Matangazo ya kibiashara

Mpango alionekana siku ya Jumapili baada ya kukosekana kuonekana hadharani kwa zaidi ya kipindi cha mwezi moja, hatua ambayo ilimaliza madai kwenye mitandao ya kijamii kuwa huenda alikuwa amefariki.

Waziri wa habari Nape Nnauye ameagiza kuchunguzwa kwa wote waliohusika kwa kusambaza madai hayo.

Dkt Mpango kwa upande wake ameeleza kuwa aliathirika na taarifa hizo za kupotosha na za uongo kwenye mitandao ya kijamii.

 

Naibu huyo wa rais alionekana mwisho kwenye umma tarehe 31 ya mwezi Oktoba wakati akimwakilisha rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao wa kijamii wa wakuu wa nchi za SADC.

Kutokuwepo kwake katika majukuwa ya umma kumezua wasiwasi mkubwa, huku waziri mkuu Kassim Majaliwa awali akiwaonya wananchi dhidi ya uvumi kuhusu kifo chake.

Makamu huyo wa rais alionekana kwenye ibada ya Jumapili katika mji mkuu, Dodoma, ambapo alisema kwamba alikuwa mzima wa afya.

 

 

"Kumekuwa na picha zinazozunguka kando ya mshumaa, na kudai kuwa nimeaga dunia. Ni mapema sana - sijamaliza kazi ambayo Mungu alinituma kufanya," Mpango alisema.

"Nitarudi kwa Muumba wangu tu wakati wangu utakapofika. Ninashukuru kwa maombi yako."

Alifafanua kuwa amekuwa nje ya nchi kwa "majukumu maalum", bila kutoa maelezo zaidi.

Waziri wa habari aliviagiza vyombo vya dola kuwachukulia hatua wale wanaoeneza uvumi kuhusu mahali alipo makamu wa rais.

Hii si mara ya kwanza kuzuka uvumi kuhusu hali ya afya ya naibu huyo wa rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.