Pata taarifa kuu

Tanzania: Ishirini waangamia kutokana na maporomoko ya ardhi kaskazini mwa nchi

Takriban watu 20 wamefariki na wengine 70 kujeruhiwa katika maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa kaskazini mwa Tanzania, kamishna wa wilaya iliyoathiriwa amesema siku ya Jumapili, Desemba 3, akihakikisha kwamba idadi ya watu inaweza kuongezeka. 

Baada ya kukumbwa na ukame ambao haujawahi kushuhudiwa, Afrika Mashariki imekumbwa na mvua kubwa kwa wiki kadhaa na mafuriko yanayohusishwa na mfumo wa hali ya hewa ya El Nino, ambayo imesababisha zaidi ya watu milioni moja kuyahama makazi yao nchini Somalia na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 300 katika eneo hilo. Hapa lori lililokwama katika mafuriko huko Isinya, kilomita 60 kusini mashariki mwa Nairobi, Machi 15, 2018.
Baada ya kukumbwa na ukame ambao haujawahi kushuhudiwa, Afrika Mashariki imekumbwa na mvua kubwa kwa wiki kadhaa na mafuriko yanayohusishwa na mfumo wa hali ya hewa ya El Nino, ambayo imesababisha zaidi ya watu milioni moja kuyahama makazi yao nchini Somalia na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 300 katika eneo hilo. Hapa lori lililokwama katika mafuriko huko Isinya, kilomita 60 kusini mashariki mwa Nairobi, Machi 15, 2018. TONY KARUMBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mvua kubwa imenyesha katika mji wa Katesh kaskazini mwa Tanzania tangu Jumamosi, takriban kilomita 300 kaskazini mwa mji mkuu Dodoma, amesema mkuu wa wilaya ya Hanang Janeth Mayanja, akiongeza kuwa "hadi sasa, watu 20 wamefariki na wengine sabini kujeruhiwa. "Idadi hii labda itaongezeka," amebainisha. 

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akisafiri kuelekea Dubai kwa mkutano wa tabia nchi, COP28, ametoa "rambirambi" zake, akisema "amegiza kutumwa" kwa misaada kusaidia waathiriwa. Baada ya kukumbwa na ukame ambao haujawahi kushuhudiwa, Afrika Mashariki imekumbwa na mvua kubwa kwa wiki kadhaa na mafuriko yanayohusishwa na mfumo wa hali ya hewa ya El Nino, ambayo imesababisha zaidi ya watu milioni moja kuyahama makazi yao nchini Somalia na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 300 katika eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.