Pata taarifa kuu

Uganda: Bunge limeidhinisha uzuiaji wa kuagiza mafuta kupitia Kenya

Bunge nchini Uganda limepitisha mswada unaoruhusu kampuni ya mafuta inayomilikiwa na serikali Uganda National Oil Company (Unoc) kutafuta na kusambaza mafuta katika soko la ndani.

Uganda, nchi isiyo na bandari, inaagiza zaidi ya 90% ya mafuta yake kupitia bandari ya Mombasa ya Kenya
Uganda, nchi isiyo na bandari, inaagiza zaidi ya 90% ya mafuta yake kupitia bandari ya Mombasa ya Kenya © Hajarah Nalwadda/AP
Matangazo ya kibiashara

Iwapo mswada huo utaidhinishwa na rais Yoweri Museveni, utamaliza mpango wa miongo kadhaa ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki kutegemea kampuni za Kenya kuagiza mafuta kutoka nje.

Wabunge waliounga mkono mswada huo walisema utapunguza gharama ya mafuta na kuwaondoa wafanyabiashara wa kati na makampuni ya mafuta ambayo yanaathiri na kusababisha bei ya mafuta kupanda.

Waziri wa nishati wa Uganda Ruth Nankabirwa hivi majuzi alisema kuwa nchi hiyo ilihitaji kuacha kuagiza mafuta kutoka nje kupitia makampuni ya Kenya kwani imeiweka Uganda kwenye udhaifu wa mara kwa mara wa usambazaji.

Uganda, nchi isiyo na bandari, inaagiza zaidi ya 90% ya mafuta yake kupitia bandari ya Mombasa ya Kenya na sehemu inayosalia kupitia bandari ya Dar es Salaam ya Tanzania, kulingana na waziri Nankabirwa.

Nchi hiyo pia inalenga kutumia Tanzania katika masuala yake ya usambazaji wa mafuta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.