Pata taarifa kuu

Kenya na Iran zimetia saini mikataba ya ushirkiano na biashara

Nairobi – Rais William Ruto amesema kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili bado kiko chini lakini kuna uwezekano wa kukua.

Kenya inatarajia kunufaika pakubwa katika ushirikiano wake na Iran
Kenya inatarajia kunufaika pakubwa katika ushirikiano wake na Iran © Wiliam Ruto
Matangazo ya kibiashara

Alieleza kuwa Kenya na Iran zitaweka utaratibu utakaowezesha mauzo ya nje chai, kahawa na nyama zaidi.

Kwa mujibu wa rais Ruto, hatua hii italeta uwiano wa kibiashara unaotarajiwa kati ya mataifa hayo mawili.

Rais Ruto pia ameeleza kwamba Kenya pia itatumia utajiri wa nchi hiyo ya Asia Magharibi katika teknolojia na uvumbuzi kwa maendeleo yake.

Alidokeza kwamba kuanzishwa kwa jumba la ubunifu na teknolojia la Iran mjini Nairobi kutatoa jukwaa mwafaka kwa biashara za Iran na Kenya.

Mataifa hayo mawili yamepiga hatua katika masuala ya ushirikiano katika maendeleo, elimu, ufadhili wa masomo, miundombinu, afya, maji, uvuvi na kilimo.

Wakati wa mkutano wao, rais Ruto na Raisi walishuhudia kutiwa saini kwa makubaliano mapya katika nyanja za kilimo, mifugo, utamaduni na urithi, habari, teknolojia, uvuvi, makazi, maendeleo ya mijini na miji mikuu.

Rais Ruto amesifia  uungwaji mkono wa Iran katika afya, akiitaja kuwa hatua muhimu kuelekea utimilifu wa huduma ya afya kwa wote nchini Kenya.

Naye rais Raisi alipongeza kujitolea kwa Kenya kuweka mazingira rafiki kwa biashara za kigeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.