Pata taarifa kuu

Shirika la Toastmasters linavyochangia kukuza lugha ya Kiswahili kutumia makundi yake yanayozungumza Kiswahili.

Licha ya kuwa Lugha ya Kiswahili ,imetambuliwa lugha ya kimataifa ,juhudi za kuikuza bado ni kidogo.Nchini Kenya shirika la kimataifa la  Toastmasters ,inayotoa mafunzo kuhusu namna ya kuwasiliana hadharani kwa ujasiri na uongozi,linaendesha vilabu vinavyotumia  lugha ya Kiswahili katika shughuli zake,Watabaruku na Fasaha Bilingual.

Wanachama wa ToastMasters wilaya ya 114 Afrika Mashariki
Wanachama wa ToastMasters wilaya ya 114 Afrika Mashariki © courtesy
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Toasmasters Ijapokuwa ina wanachama wengi wanaozungumza Kiingereza, ilikuja na mpango maksusi wa kuruhusu vilabu viwili vya uwili kwenye wilaya ya Afrika Mashariki ,Watabaruku na Fasaha

Emilia Siwingwa,wakili kutoka Dar Salam , ni sehemu ya uongozi uliotumika kuyazalisha makundi haya.

Katika wilaya ya Afrika Mashariki ,kuna fursa ya kumwezesha mtu mzungumzaji bora katika lugha ya Kiswahili,popote pale alipo duniani,aweze kujumuika  na kupata uzoevu,kujielezea pamoja na kuwaongoza watu wengine kwa lugha ya Kiswahili,”alisema Bi Emilia Siwingwa .

Rais wa kikundi cha Watabaraku Eric Alligator Makori, anasikitika kuwa baadhi ya raia wa Afrika Mashariki wanapata taabu kwenye matumizi ya lugha ya Kiswahili ,ambayo raia wa kigeni wanaokuja wanachangamkia na kuweza kuitumia kwa urahisi.

Kuna wanachama wengi ambao walipojiunga nasi,hawakuweza kujieleza kwa lugha ya Kiswahili hata kidogo. Mmoja wao alinieleza kuwa alikwenda kwenye mahojiano ya kazi,Arusha,baadhi ya waliomhoji ,hawakuwa wa kiasili ya Afrika lakini walikuwa wanazungumza lugha ya Kiswahili kwa kiasi,na yeye hakuweza kuzungumza lugha ya Kiswahili hata kidogo,basi hakuweza kupata kazi yenyewe. Lakini leo hii;anajieleza kwa ufasaha sana,kwa sababu amepata fursa nyingi za kuhutubu kwa lugha ya Kiswahili ,kuwaskiliza wasemaji wazuri wa lugha ya Kiswahili,”alielezea Alligator Makori ambaye pia ni bingwa wa hotuba katika mashindano ya Afrika Mashariki mwaka huu.

Caroline Kodo mwanachama wa kikundi cha Fasaha Bilingual ,anasema japo  alikuwa mwanafunzi bora wa Kiswahili,mazingira yake yalimbadilisha .

Nairobi tumezoea kusema sana kwa lugha ya Kingereza i ,hivyo basi inakuwa ni kama umesahau. ile lugha. Nilijipata  kazini Mombasa na hapo kazi yangu ikawa lazima kushirikiana na  kuwasiliana na wazee waliostaafu. Basi siku moja rafiki yangu anaitwa Wanjiru Mureithi ,akaniambia kuna kikundi cha watu wanaoitwa Toastmasters,basi nikajiungana nao mkutano mmoja  na hapo nikafurahi kuwa kwa saa mbili kila mtu alijikakamua kusema kwa lugha ya Kiswahili.

Lugha ya Kiswahili inazungumzwa na watu zaidi ya  miloni 200 duniani pia lugha rasmi ya umoja wa Afrika .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.