Pata taarifa kuu

Idadi ya vifo vya ajali ya barabarani Kenya yapanda hadi 49

Idadi ya vifo kutokana na ajali mbaya ya barabarani Magharibi mwa Kenya imeongezeka na kufikia watu 49. Waokoaji walikuwa na wakati mgumu kuyaondoa mabaki ambapo waathiriwa zaidi walihofiwa kunaswa. Ajali hiyo mbaya ya barabarani imetokea kwenye makutano ya magari nchini Kenya, polisi na walioshuhudia wamethibitisha.

Ajali hiyo ilitokea kwenye barabara kuu kati ya mji wa Nakuru na Kericho. Mkuu wa Mkoa wa Bonde la Ufa Abdi Hassan amesema zaidi ya watu 30 pia walijeruhiwa wakati lori hiyo ilipoyagonga magari madogo, bodaboda na vibanda vya wauzaji.
Ajali hiyo ilitokea kwenye barabara kuu kati ya mji wa Nakuru na Kericho. Mkuu wa Mkoa wa Bonde la Ufa Abdi Hassan amesema zaidi ya watu 30 pia walijeruhiwa wakati lori hiyo ilipoyagonga magari madogo, bodaboda na vibanda vya wauzaji. AP
Matangazo ya kibiashara

Ajali hiyo ilitokea baada ya lori lililokuwa limebeba kontena kupoteza mwelekeo  katika eneo la Londiani, karibu na mji wa magharibi wa Kericho, ripoti ya vyombo vya habari vya ndani zimeeleza.

Ajali hiyo ilitokea kwenye barabara kuu kati ya mji wa Nakuru na Kericho. Mkuu wa Mkoa wa Bonde la Ufa Abdi Hassan amesema zaidi ya watu 30 pia walijeruhiwa wakati lori hiyo ilipoyagonga magari madogo, bodaboda na vibanda vya wauzaji.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi katika eneo kulikotokea ajali, Geoffrey Mayek, watu  wengine 30 walijeruhiwa vibaya ambapo idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka.

Madereva nchini humo wametakiwa kuwa waangalifu wanapokuwa barabarani haswa msimu huu wa mvua
Madereva nchini humo wametakiwa kuwa waangalifu wanapokuwa barabarani haswa msimu huu wa mvua AP

Licha ya kuwepo kwa hofu kuwa idadi ya waliofairki katika ajali hiyo inaweza kuongezeka, inadaiwa kuwa huenda kuna watu ambao wanaweza kuwa wamenaswa chini ya gari lililopinduka.

Walioshuhudia waliambia vyombo vya habari vya Kenya kuwa dereva huyo alikuwa akijaribu kulikwepa basi lililokuwa limeharibikia barabarani.

Rais wa Kenya William Ruto alisema amehuzunishwa kusikia kwamba baadhi ya waliouawa walikuwa "vijana wenye kujituma kwa ajili ya ujenzi wa taifa na wafanyabiashara ambao walikuwa kwenye shughuli zao za kila siku".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.