Pata taarifa kuu
KENYA-USALAMA

Kenya: Watu 20 wafariki dunia katika basi lililosombwa na mto Enziu

Zaidi ya watu 20 walikufa maji Jumamosi hii Desemba 4 wakati basi lao lililokuwa likielekea kwenye harusi liliposombwa na Mto Enziu uliofurika maji kwenye daraja moja katikati mwa Kenya, polisi imesema.

Moja ya mitaa ya Nairobi, Kenya. Basi hilo lilizama kwenye Mto Enziu, takriban kilomita 200 mashariki mwa jiji kuu la Nairobi, haikujulikana mara moja.
Moja ya mitaa ya Nairobi, Kenya. Basi hilo lilizama kwenye Mto Enziu, takriban kilomita 200 mashariki mwa jiji kuu la Nairobi, haikujulikana mara moja. SOPA Images/LightRocket via Gett - SOPA Images
Matangazo ya kibiashara

Wapita njia wamepiga kelele wakati basi la shule ya manjano lililokodiwa kusafirisha wanakwaya ya kanisa na wengine kwenye hafla iliyopangwa katika Kaunti ya Kitui lilipinduka na kuzama dereva akijaribu kujaribu kuongoza basi lake kwenye kinakirefu cha maji.

Baadhi ya watu waliokuwa kwenye basi hilo walifanikiwa kujiokoa kabla ya basi kuzama katika maji na kupelekwa mahali salama. "Tulipata ajali hii mbaya iliyotokea hapa asubuhi ya leo," gavana wa Kitui Charity Ngilu amewaambia wanahabari.

Ameongeza kuwa "miili 23" hadi sasa ilikuwa imetolewa mtoni na "bado kuna miili kwenye basi". Amesema shughuli ya kuitafuta miili ya waathiriwa itaanza tena Jumapili asubuhi. Bi Ngilu amesema watu 12 waliokolewa wakiwemo watoto 4. Idadi kamili ya abiria waliokuwa kwenye basi hilo lilipozama kwenye Mto Enziu, takriban kilomita 200 mashariki mwa jiji kuu la Nairobi, haikujulikana mara moja.

Basi hilo lilikuwa likiwasafirisha wakwaya wa kanisa na wanakijiji waliokuwa wakkenda harusini wakati wa ajali hiyo. Walioshuhudia wamesema kuwa dereva wa basi hilo alijaribu kuvuka daraja, huku likiwa limefurika kwa maji, ambayo nguvu yake ilisomba gari hilo katika mkondo wa mzunguko. Makamu wa Rais William Ruto ametoa rambirambi zake kwa familia za waathiriwa, huku akiwataka madereva wa magari kuchukua tahadhari zaidi katika barabara za Kenya, ambako maeneo mengi kwa sasa yanakumbwa na mvua kubwa

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.