Pata taarifa kuu

Tanzania yaondoa marafuku ya usafiri wa usiku

Nairobi – Tanzania imeondoa marufuku ya usafiri wa mabasi ya usiku ambayo iliwekwa miongo kadhaa iliyopita. 

Tanzania yaondoa marafuku ya usafiri wa usiku
Tanzania yaondoa marafuku ya usafiri wa usiku © UDA RAPID TRANSIT PLC
Matangazo ya kibiashara

Serikali inasema mabadiliko hayo yamekuja baada ya kuzingatia maoni ya wadau wa sekta ya usafiri, pamoja na uboreshaji wa miundombinu na usalama. 

Wakati akitangaza hatua hiyo bungeni, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema marafuku hiyo iliekwa miaka ya 1990 kufuatia kuongezeka kwa ajali za barabarani na utekaji wa mabasi. 

Majaliwa ameziagiza mamlaka husika kufanya kazi ya “kuweka utaratibu utakaofuatwa na wamiliki na madereva wa mabasi ya abiria wanaokusudia kusafirisha abiria usiku”. 

Hatua hiyo inatarajiwa kuchochea ukuaji wa sekta ya usafiri na imepokelewa kwa furaha na chama cha wamiliki wa mabasi nchini humo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.