Pata taarifa kuu

Viongozi wa kikanda wamekutana Luanda kujadili usalama mashariki ya DRC

Nairobi – Viongozi kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, SADC, Jumuiya ya Afrika ya Kati na eneo la Maziwa Makuu, ICGLR chini ya Umoja wa Afrika, walikutana jana jijini Luanda nchini Angola kujadili hali ya usalama Mashariki mwa DRC

Wakuu wa ukanda wameahidi kuendelea kuisaidia nchi ya DRC kupambana na makundi ya waasi
Wakuu wa ukanda wameahidi kuendelea kuisaidia nchi ya DRC kupambana na makundi ya waasi © RDC
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano huo, viongozi hao wamepogeza hatua za kisiasa na kijeshi zinazofanyika kujairbu kurejesha amani ya kudumu Mashariki mwa DRC licha ya changamoto zinzoendelea, ikiwemo watu waliokimbia makaazi yao kuendelea kukabiliwa na ukosefu wa mahitaji muhimu ya binadamu.

Mkutano huo pia umempongoza rais Felix Thisekedi wa DRC na Paul Kagame wa Rwanda kwa kuonesha nia ya kutumia njia ya mazungumzo ili kumaliza toafauti kati ya nchi hizo mbili, na kusaidia kupata amani Mashariki mwa DRC.

Mkutano huo pia umepongzea jithada zinazofanywa na kikosi cha pamoja cha nchi za Afrika Mashariki, kurejea utulivu na amani katika maeneo yaliyokuwa chini ya waasi wa M23.

Pia wameunga mkono jitihada za Jumuiya za EAC, ECCAS, ICGLR na SADC kuja na mbinu za pamoja kusaidia kupata uthabiti Mashariki mwa DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.