Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Waziri wa Kenya awaita waandishi wa habari 'makahaba'

Waziri wa biashara wa Kenya amekumbwa na msukosuko siku ya Jumatano baada ya kukashifu hadharani kundi la wanahabari, akiwashutumu kwa kuegemea upande wa upinzani na kuwaita waandishi hao 'makahaba'.

Rais William Ruto, ambaye alishinda kwa kura chache katika uchaguzi wa urais mwaka jana dhidi ya Bw Odinga, siku za nyuma alivishutumu vyombo vya habari kwa kutangaza habari zinazoegemea upande mmoja.
Rais William Ruto, ambaye alishinda kwa kura chache katika uchaguzi wa urais mwaka jana dhidi ya Bw Odinga, siku za nyuma alivishutumu vyombo vya habari kwa kutangaza habari zinazoegemea upande mmoja. © REUTERS/Michele Tantussi
Matangazo ya kibiashara

Upinzani na vyama vya wanahabari vimetoa wito wa kumsusia waziri, Moses Koria, wakibaini kwamba baada ya matamshi hayo, hastahili kufanya kazi katika serikali.

Katika hafla ya hadhara siku ya Jumapili, Bw. Koria alishambulia Nation Media Group (NMG), mojawapo ya vyombo vikubwa vya habari Afrika Mashariki, inayomilikiwa na Aga Khan. Hasa, alitishia kumfukuza kazi afisa yeyote wa serikali ambaye alifanya biashara na NMG, akihoji kama NMG ni chombo cha habari 'au chama cha upinzani'.

Katika ujumbe wake wa Twitter uliotumwa kwa Kiswahili, pia aliwataja "makahaba wa Aga Khan", akimaanisha waandishi wa habari wa kundi hilo, akisema "walikiri kulazimishwa na wakuu wao na wasimamizi kuandika makala dhidi ya serikali kama sehemu ya mpango uliofadhiliwa na rais wa zamani".

NMG ilijibu kwa kubaini kwamba maneno ya waziri aliyatoa baada ya matangazo ya Jumapili kwenye mojawapo ya vituo vyake, NTV, ya ripoti ya uchunguzi kuhusu uwezekano wa sakata inayohusishwa na uagizaji bidhaa ndani ya wizara ya Bw. Koria. 'Shambulio la maneno' la Bw. Koria 'sio tu kwamba halifai kwa mtu kama yeye, pia ni shambulio dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari, msingi wa demokrasia", ilijibu siku ya Jumanne katika tahariri ya Gazeti la Daily. Nation, mojawapo ya magazeti makuu ya kila siku nchini, yanayomilikiwa na NMG.

Seneta wa upinzani, Edwin Sifuna, aliwasilisha pendekezo la kutokuwa na imani na Bw. Koria wiki hii, akibaini kuwa mashambulizi dhidi ya chombo cha habari "mara nyingi husababisha mashambulizi dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari kwa jumla". Mnamo Jumatano, wanachama wa chama cha kiongozi wa upinzani Raila Odinga waliondoka kwenye kikao cha Bunge la Seneti kupinga kuwasili kwa Bw. Koria, na kupinga marufuku ambayo walipewa kumuuliza maswali.

"Sitaomba msamaha," Bw. Koria amejibu kwa vyombo vya habari siku ya Jumatano.

Rais William Ruto, ambaye alishinda kwa kura chache katika uchaguzi wa urais mwaka jana dhidi ya Bw Odinga, siku za nyuma alivishutumu vyombo vya habari kwa kutangaza habari zinazoegemea upande mmoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.