Pata taarifa kuu
UCHUNGUZI-HAKI

Mahakama yatangaza kuwa Félicien Kabuga 'hastahili' kushtakiwa kwa sababu za kiafya

Hakutakuwa na kesi katika mahakama ya The Hague kuhusu Rwanda kwa Félicien Kabuga. Kesi hiyo iliyoanza Septemba 2022 mbele ya Mfumo wa kimataifa wa kushughulikia mabaki ya kesi za mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994. Mahakama ilitaka kuchunguza hali ya afya ya akili ya mtu ambaye anachukuliwa kuwa mfadhili wa mauaji ya halaiki nchini Rwanda mwaka wa 1994. Majaji wameamua, Félicien Kabiuga hastahili kushtakiwa.

Picha ya Félicien Kabuga, wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake huko Hague, Agosti 18, 2022. Imechukuliwa kutoka kwa rekodi ya video ya Mfumo wa kimataifa unaosimamia kesi za mwisho za Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa Rwanda, ICTR.
Picha ya Félicien Kabuga, wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake huko Hague, Agosti 18, 2022. Imechukuliwa kutoka kwa rekodi ya video ya Mfumo wa kimataifa unaosimamia kesi za mwisho za Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa Rwanda, ICTR. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Hague, Stéphanie Maupas

Félicien Kabuga hafai kujibu mashtaka na hakuna uwezekano wa kurejesha uwezo wake wa kimwili. Ilichukua miezi mitatu tangu kusimamishwa kusikilizwa kwa mashahidi wa mwendesha mashtaka kwa majaji kuamua. Wataalamu kadhaa waliegemea kando ya kitanda cha mshtakiwa, walikuja kutoa ushahidi huko Hague. Wanasaikolojia wawili na daktari wa neva walifanya uchunguzi wa shida ya akili ya asili ya mishipa.

Kesi bado haijafungwa

Hata kama hastahili kushtakiwa, hilo halifungi kesi. Félicien Kabuga hataachiliwa. Mfanyabiashara huyo wa zamani atasalia chini ya uangalizi wa kimatibabu, kama alivyokuwa tangu alipowasili Hague mwezi Oktoba 2020. Majaji wameweka utaratibu maalum unaofanana na utaratibu wa kutafuta ukweli ambao anatuhumiwa.

Hakuna hukumu ya hatia

Mwendesha mashtaka atalazimika kuendelea kuwasilisha ushahidi wake mbele ya majaji, kujaribu kuthibitisha kwamba Félicien Kabuga alikuwa na nia ya kufanya mauaji ya halaiki, yaani kuangamiza Watutsi. Lakini utaratibu huu hauwezi kusababisha hatia. Hakuna hukumu ya hatia inayoweza kutolewa dhidi ya Félicien Kabuga. Lakini kwa macho ya majaji, hii itawezesha kufunga kesi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.