Pata taarifa kuu

Kenya na Ufaransa zazindua mradi wa kupambana na moto kwenye misitu

NAIROBI – Waziri wa Ufaransa anayehusika na maendeleo ya kimataifa, Chrysoula Zacharopoulou, hivi leo ameongoza ujumbe wa Ufaransa  na umoja wa Ulaya nchini Kenya, kuzindua mradi wa kupambana na moto katika misitu.

Kenya na Ufaransa zimezindua mradi wa kupambana na majanga ya moto kwenye misitu
Kenya na Ufaransa zimezindua mradi wa kupambana na majanga ya moto kwenye misitu © French Embassy kenya
Matangazo ya kibiashara

Mradi huo utakaogharimu euro milioni 22, tayari uko katika awamu ya kwanza na unatarajiwa kuisaidia Kenya katika malengo yake ya kuafikia asilimia 30 ya misitu kufikia 2030.

Alex Lemarkoko ni mhifadhi mkuu kutoka wakala wa huduma za misitu nchini Kenya.

“Huu mradi unatupa uwezo katika shirika la misitu nchini Kenya kwa kutuwezesha kupata ripoti kwa mapema na kuweza kushugulikia moto.” ameeleza Alex Lemarkoko.

00:19

Alex Lemarkoko, mhifadhi mkuu kutoka wakala wa huduma za misitu nchini Kenya

Mbali na kutumia timu ya maafisa wa KFS kwenye mradi huu, Alex anasema wanalenga pia kuzishirikisha jamii zinazoishi karibu na misitu.

“Sheria inatukubali kufanya kazi na jamii na hilo tumekuwa tukifanya swala tu ambalo tumekosa kufanya ni kutoa mafunzo na kwa sasa mradi huu utatusaidia kuwapa raia maarifa zaidi. ” alielezea Alex Lemarkoko. 

00:29

Alex Lemarkoko kuhusu ushirikiano na jamii

Naye waziri Chrysoula, amesema Ufaransa na umoja wa ulaya zitaendelea kuunga mkono miradi mingine ikiwemo kutoa elimu kwa vijana kuhusu uhifadhi.

“Mradi huu ni mfano mwingine wa ushirikiano wetu, na bilashaka inatilia mkazo lengo la serikali ya Kenya kuhakikisha nchi ina asilimia 20 ya misitu kufikia 2023; kwa kuimarisha juhudi za kupamabana moto kwenye misitu, kuimarisha uwezo wa KFS katika ufuatiliaji na mawasiliano na kuchagia katika agenda kuu ya serikali kuhusu mabadiliko ya tabianchi na bayoanuai.” amesema Chrysoula Zacharopoulou.

00:25

Chrysoula Zacharopoulou, Waziri wa Ufaransa anayehusika na maendeleo ya kimataifa

Mpaka sasa Kenya imepoteza hekari zaidi la laki 1 na elfu 35 kutokana na moto, ambapo mradi huu utahusisha matumizi ya vifaa kama vile ndege zisizo na rubani na vifaa vya kugundua moto haraka na kuwezesha maafdia wa KFS kuuzima kwa wakati. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.