Pata taarifa kuu

Wanajeshi wa SADC  kupelekwa Mashariki mwa DRC mwanzoni mwa mwezi ujao

NAIROBI – Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kupitia wizara ya mambo ya nje imethibitisha kuwa vikosi vya wanajeshi wa SADC vitaanza kuwasili katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo ifikapo mwanzoni mwa mwezi Ujao.

Marais wa nchi wanachama wa Muungano wa SADC, Mei 8, nchini Namibia.
Marais wa nchi wanachama wa Muungano wa SADC, Mei 8, nchini Namibia. © @SADC_News
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari waziri wa mambo ya nje wa DRC Christophe Lutundula amesema kuwa katika mkutano wa kilele uliofanyika mjini Windhoek, Namibia mei 08    nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC, zilikubaliana kwa pamoja kutoa msaada wa kijeshi kwa DRC.

Kwa mujibu Lutundula Kikosi ambacho kitapelekwa huko Kivu Kaskazini, mashariki mwa nchi hiyo, kwanza kitakabidhiwa kanuni za kusaidia juhudi za upatikanaji wa usalama hasa katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa M23 ambao wameteka sehemu ya jimbo hilo.

Bila ya kutoa maelezo zaidi kuhusu kanuni hizo, wala muundo wa kikosi hicho, waziri Lutundula amefahamisha kuwa maandalizi ya kuwapokea wanajeshi wa SADC yanaendelea huku Chanzo kilicho karibu na serikali ya Kinshasa kikithibitisha kuwa majadiliano yanaendelea.

Kikosi hicho kinaweza kufika DRC kati ya Juni 15 na 20, alisema waziri huyo huku akijua kuwa mamlaka ya EAC yanakaribia kumalizika.

Haya yanajiri wakati Mkutano wa Kimataifa wa Nchi za Maziwa Makuu ukitarajiwa kufanyika Juni 3 ambapo Umoja wa Afrika unapaswa kusimamia kinadharia mkutano wa kilele wa pande nne na EAC, SADC, ICGLR na mikataba ya Addis Ababa kuhusu hali ya Mashariki mwa DRC katika wiki zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.