Pata taarifa kuu

Namibia: Kikao cha SADC kinafanyika kujadili usalama wa mashariki ya DRC

NAIROBI – Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) inakutana Jumatatu hii, Mei 8, 2023 nchini Namibia kwa ajili ya Mkutano wa pande 3 maarufu Troika.

Mkutano wa nchi za SADC unafanyika nchini Namibia kujadili suala la usalama wa DRC
Mkutano wa nchi za SADC unafanyika nchini Namibia kujadili suala la usalama wa DRC (Photo : Wikipédia)
Matangazo ya kibiashara

Troika Ni chombo kinachosimamia masuala ya ulinzi na usalama ya shirika hilo la kikanda, ambalo kwa sasa linaongozwa na rais wa DRC Felix Tshisekedi. Pia atakuwepo Windhoek, hasa kwa vile mkutano huu lazima ulenge zaidi mzozo wa mashariki mwa nchi.

Lengo hasa la mkutano huu kwa DRC ni kukazia ombi lake la kutaka kuungwa mkono kijeshi na jumuiya hiyo katika mzozo na waasi wa M23, ambapo tayari Angola imekwisha onyesha nia ya kuunga mkono pendekezo hilo, Lakini Kinshasa inataka uwazi zaidi kwa majirani yake kuhusu swala hili.

Duru kutoka Ikulu ya Kinshasa zinasema kuwa serikali inampango wa kubadili mamlaka ya vikosi vya Jumuiya ya Afrika mashariki nchini DRC kwa kuvipa mamlaka ya kushambulia na hakuna haja ya kuwa na viksoi vya kukaa kati kwa kati. Lakini changamoto kubwa kuhusu hili ni kuishawishi Afrika Kusini.

Kando na mkutano wa ICGL uliofanyika jijini Bujumbura jumamosi iliopita kuhusu DRC, Felix Tshisekedi alijadiliana na rais Cyril Ramaphosa. Wataalamu wanaona kuwa kinachoelekea ni kutafuta kufufua upya brigade ya kuingilia kati mashambulizi ya waasi iliofaulu kuwasambaratisha M23 mwaka 2013.

Juhudi za kidiplomasia zinaendelea juma hili, ambapo baada ya Windhock rais Felix Tshisekedi ataelekea Botswana kwa safari ya kikazi ya siku kadhaa ambapo atazuri makao makuu ya SADC yaliop okatika mji mkuu Gaborone.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.