Pata taarifa kuu

Maandamano nchini Kenya: Rais Ruto atangaza kupunguzwa kwa bei ya unga

Rais wa Kenya William Ruto alitangaza Ijumaa kushuka kwa bei ya unga wa mahindi, chakula kikuu katika nchi hii ya Afrika Mashariki iliyotikiswa mwishoni mwa mwezi Machi kutokana na maandamano ya kupinga mfumuko wa bei na gharama ya maisha.

Rais wa Kenya William Ruto, Machi 28, 2023.
Rais wa Kenya William Ruto, Machi 28, 2023. REUTERS - MICHELE TANTUSSI
Matangazo ya kibiashara

Siku tatu za maandamano kwa mwito wa mpinzani Raila Odinga zilizua uporaji na makabiliano na polisi na kusababisha vifo vya watu watatu. "Najua tuna tatizo na gharama ya maisha. Mwishoni mwa wiki ijayo, bei ya unga (unga wa mahindi) itashuka kutokana na kuwasili kwa unga kutoka nje," mkuu wa nchi alisema siku ya Ijumaa.

William Ruto aliyechaguliwa mnamo Agosti 2022 amekuwa akikabiliwa na ukosoaji, hasa baada ya kuondoa ruzuku ya gharama kubwa ya mafuta na unga wa mahindi, ambayo bei yake imeongezeka.

Kenya ambayo ni kiungo muhimu wa Uchumi Afrika Mashariki, inakabiliwa na mfumuko wa bei unaozidi kuimarika, ambao ulifikia 9.2% katika kipindi cha mwaka mmoja mwezi Februari. Bei za vyakula pekee ziliongezeka kwa asilimia 13.3. Kiongozi mkuu wa upinzani Raila Odinga aliandaa maandamano ya siku tatu, Machi 20, 27 na 30, dhidi ya serikali ya William Ruto, ambaye anaituhumu kuiba uchaguzi wa urais wa 2022 na kushindwa kudhibiti mlipuko wa Gharama ya maisha.

Mikutano hii ilizua uporaji na makabiliano na polisi katika vitongoji duni katika mji mkuu Nairobi na vile vile katika mji wa Kisumu, ngome ya Odinga magharibi mwa nchi na kusababisha vifo vya watu watatu. Kisha Bw Odinga alisitisha mwito wake wa maandamano ya kila wiki mbili, baada ya William Ruto kupendekeza mazungumzo bungeni.

Lakini mpangilio wa mijadala hii ni chanzo cha mvutano. Chama cha Odinga, Azimio, kinataka waangalizi kutoka nje ya bunge kuhusika katika mazungumzo hayo, mhoja ambayo serikali imefutilia mbali. Raila Odinga alitishia kuingia barabarani tena ikiwa hakufurahishwa na mchakato huo, akisema tarehe zaidi za maandamano zinaweza kutangazwa baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kukamilika Alhamisi ya wiki ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.