Pata taarifa kuu

Kipindupindu nchini DRC: 'Hali ya ya kibinadamu inaanza kuwa shwari'

Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kesi 3,200 za kipindupindu zilirekodiwa mnamo Januari 2023, robo tatu yao kati ya watu nusu milioni waliokimbia makazi huko Kivu Kaskazini. 

Watoto wa shule wakipita mbele ya mabango yanayoelezea dalili, hatari na tahadhari za ugonjwa wa kipindupindu mjini Kinshasa Januari 18, 2018.
Watoto wa shule wakipita mbele ya mabango yanayoelezea dalili, hatari na tahadhari za ugonjwa wa kipindupindu mjini Kinshasa Januari 18, 2018. AFP - JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara

Kipindupindu kimekuwa kikiongezeka tena barani Afrika tangu mwanzoni mwa 2023. Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilirekodi visa vipya 26,000 katika nchi kumi za bara hilo mnamo Januari 2023 pekee.

Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambayo ilirekodi kesi 3,200 mnamo mwezi Januari, ikiwa ni pamoja na robo tatu kati ya watu nusu milioni waliokimbia makazi huko Kivu Kaskazini, janga hilo linatulia kutokana na mpango wa kukabiliana. Lakini wa pili wanakosa ufadhili na hali inabaki kuwa tete.

"Tuliomba chanjo haraka, na tukamaliza duru ya kwanza," alisema Daktari Placide Welo Okitayemba, mkurugenzi wa mpango wa kutokomeza kipindupindu katika Wizara ya Afya ya Kongo. Kuna zaidi ya watu 340,000 waliochanjwa, hasa katika maeneo haya mawili ya afya ambapo kuna watu waliokimbia makazi yao huko Nyiragongo na Karisimbi”.

Ukosefu wa uwezo, hasa katika upatikanaji wa maji, usafi wa mazingira, na usafi

Anaongeza: “Ninaamini kuwa hali katika suala la janga hili inatengemaa. Tunaanzisha vitendo vya jumuiya ili kujaribu kupunguza mlolongo wa maambukizi. Tulitoka kwa kesi 200 kwa siku hadi wastani wa kesi 33 kwa siku. Kwa hivyo ni hali inayoendelea vizuri, lakini yenye hatari nyingi, kwa kuwa mahitaji katika WASH [neno linalobainisha ufikiaji wa maji, usafi wa mazingira, na usafi, ] hayajashughulikiwa. »

Na daktari Placide Welo Okitayemba alibainisha: "Kila mwezi, inachukua zaidi ya dola 500,000 kupata maji, mahitaji yanayoonyeshwa kwa zaidi ya 3,250 m3 kwa siku, kwa hiyo ni kazi kubwa sana, na ambayo inahitaji msaada kutoka nje ili kuruhusu kipindupindu hiki kwa ufanisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.