Pata taarifa kuu

DRC: Askari mmoja afariki na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya helikopta ya UN kufyatuliwa risasi

Askari mmoja wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC kutoka Afrika Kusini aliuawa na mwingine kujeruhiwa vibaya Jumapili Februari 5 wakati helikopta yao ilipokabiliwa na mashambulizi ya risasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kulingana na msemaji wa Umoja wa Mataifa.

Askari mmoja wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC kutoka Afrika Kusini aliuawa na mwingine kujeruhiwa vibaya Jumapili Februari 5 wakati helikopta yao ilipokabiliwa na mashambulizi ya risasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kulingana na msemaji wa Umoja wa Mataifa.
Askari mmoja wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC kutoka Afrika Kusini aliuawa na mwingine kujeruhiwa vibaya Jumapili Februari 5 wakati helikopta yao ilipokabiliwa na mashambulizi ya risasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kulingana na msemaji wa Umoja wa Mataifa. © AFP - ALEXIS HUGUE/AFP
Matangazo ya kibiashara

Ilikuwa saa nane na nusu saa za Afrika ya Kati wakati helikopta ya Oryx kutoka MONUSCO, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, ilipigwa risasi ilipokuwa ikirejea kutoka kwa misheni huko Beni.

Katika helikopta hiyo, kulikuwepo askari watatu kutoka Afrika Kusini. Mhandisi wa ndege aliuawa, huku rubani akipata jeraha la mkono. Na rubani msaidizi ndiye alichukua hatua mikononi mwake na kufanikiwa kutua ndege katika uwanja wa kimataifa wa Goma.

Kwa mujibu wa duru za kuaminika kutoka jeshi, ndege hiyo ilishambuliwa kaskazini mwa Goma ikiwa imebeba risasi na vifaa ingine vya kijeshi.

Mapigano kati ya jeshi na M23

Bado kwa mujibu wa chanzo hicho, silaha iliyotumika na eneo kamili la tukio bado halijajulikana. Hata hivyo inaweza kuwa silaha ndogo ilitumika kwa shambulio hilo. Uchunguzi utaanzishwa mara tu walionusurika watakaposikilizwa.

Tangu Novemba 2021, waasi wa M23 wengi wao kutoka jamii ya Watutsi wameteka maeneo ya kaskazini mwa Goma. DRC inaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono, jambo ambalo linaungwa mkono na wataalamu wa Umoja wa Mataifa na mataifa ya Magharibi, lakini Kigali inakanusha hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.