Pata taarifa kuu
AMANI-MARIDHIANO

Sudan Kusini: Papa Francis awasili Juba, baada ya ziara yake nchini DR Congo

Baada ya ziara yake mjini Kinshasa, Papa Francis amewasili saa 8:52 mchana (kwa saa za nchini Sudan Kusini)  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini.

Papa Francis aliwasili katika ziara ya siku tatu nchini Sudan Kusini Februari 3, 2023 ili kuendeleza amani na maridhiano katika nchi hiyo changa zaidi duniani, inayokumbwa na misukosuko ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na umaskini uliokithiri.
Papa Francis aliwasili katika ziara ya siku tatu nchini Sudan Kusini Februari 3, 2023 ili kuendeleza amani na maridhiano katika nchi hiyo changa zaidi duniani, inayokumbwa na misukosuko ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na umaskini uliokithiri. AFP - TIZIANA FABI
Matangazo ya kibiashara

Papa Francis amewasili katika ziara ya siku tatu nchini Sudan Kusini Februari 3, 2023 ili kuendeleza amani na maridhiano katika nchi hiyo changa zaidi duniani, inayokumbwa na misukosuko ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na umaskini uliokithiri.

Kiongozi wa kanisa Katolika anaungana na askofu mkuu wa Canterbury, Justin Welby, pamoja na msimamizi wa Kanisa la Scotland, Iain Greenshields, kwa "hija ya kiekumene ya amani" nchini Sudan Kusini, ambayo itadumu hadi Jumapili.

Baada ya hafla fupi ya kuwakaribisha katika uwanja wa ndege, papa na washiriki wengine wawili wa kidini wataelekea kwenye ikulu ya rais, ambapo watakutana kwanza na Rais Salva Kiir, kisha na makamu wa rais watano wa nchi hiyo, kabla ya kuendelea na programu yao ambayo inajumuisha mikutano na mashirika ya kiraia pamoja na watu waliohamishwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, sala ya kiekumene na misa katika Makaburi ya John Garang.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.