Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI: ZIARA YA PAPA FRANCIS

Papa Francis asuburiwa Sudan Kusini

Kanisa katoliki nchini Sudan Kusini, hivi leo limefanya ibada maalumu kwa ajili ya kumkaribisha Papa Francis, ambaye anatarajiwa kuwasili nchini humo kwa ziara hapo kesho.

Papa Francis, Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani
Papa Francis, Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani AP - Alessandra Tarantino
Matangazo ya kibiashara

Papa Francis anatarajiwa kuwasili nchini humo akitokea nchini Jamuhiri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako amekuwa na ziara ya siku 3, ambapo hapo jana alifanya misa iliyoshuhudhuriwa na watu zaidi ya milioni moja jijini Kinshasa.

Kwa mujibu wa askofu wa kanisa hilo, Stephen Ameyu Martin, ibada hiyo itafanyika katika jumba la makumbusho la kiongozi wa zamani wa taifa hilo, hayati John Garanga, mjini Juba.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, ibada hiyo iliongozwa na balozi wa Vatican nchini humo, askofu Hubertus van Megan.

Katika hatua nyingine, Serikali imesema imesambaza zaidi ya maofisa usalama elfu 5 kutoka jeshi la Polisi katika jiji kuu la Juba, kuhakikisha usalama kwa Papa Francis.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.