Pata taarifa kuu

DRC: Wanajeshi wa UN wawatelekeza wanawake wajawazito na watoto wasio na baba

Katika baadhi ya matukio, askari wa Umoja wa Mataifa wamefanya mapenzi na wasichana wenye umri wa chini ya miaka 14 au 15 ili kuahidiwa ndoa, pesa au zawadi ndogo.

Mmoja wa Walinda amani wa Umoja wa Mataia kutoka Uruguay: "wapatanishi" mara nyingi walikuwa wavulana wadogo ambao walikuwa "wakizunguka kambi" na kufanya kazi kama watumwa kati ya baadhi ya wanajeshi wa MONUSCO na baadhi ya wasichana.
Mmoja wa Walinda amani wa Umoja wa Mataia kutoka Uruguay: "wapatanishi" mara nyingi walikuwa wavulana wadogo ambao walikuwa "wakizunguka kambi" na kufanya kazi kama watumwa kati ya baadhi ya wanajeshi wa MONUSCO na baadhi ya wasichana. MONUSCO/Abel Kavanagh
Matangazo ya kibiashara

Kwa rangi yake nzuri, Chance mwenye umri wa miaka 16 anatofautiana na wanafunzi wengine wa shule yake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Yeye ni mmoja wa watoto wa Kongo waliozaliwa na walinda amani kutoka kikosi cha Umoja wa Mataifa kilichopo nchini DRC kwa zaidi ya miaka ishirini.

“Nilikuwa na uhusiano mwaka 2006 na raia wa Uruguay ambaye nilimpenda sana... Nilikuwa na ujauzito wa miezi miwili alipoondoka DRC bila kuniaga,” anasema mama yake Chance, Faida, 45.

Wakati huo, Faida alikuwa mfanyakazi wa nyumba katika moja ya kambi mbili za MONUC (tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC wakati huo), ambayo ilikuja kuwa MONUSCO mwaka 2010, huko Kavumu, kilomita 30 kaskazini mwa Bukavu, mji mkuu wa Kusini, moja ya mikoa ya DRC inayokumbwa na ghasia kutoka kwa makundi yenye silaha.

Shirika la habari la AFP lilikutana na wanawake wanne huko Kavumu wakidai kuwa na watoto wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa, hali inayotambulika, ambayo ilisababisha Umoja wa Mataifa kuanzisha mwaka 2012 kanuni za "maadili ya wafanyakazi" na kusaidia familia zinazohusika, ikiwa ni pamoja na malipo ya shule (ada kwa watoto).

Wanawake hawa hawaripoti ukatili, lakini baadhi yao walikuwa na umri wa kati ya miaka 14 na 15 walipofanya mapenzi na askari hao, kwa ahadi ya ndoa, pesa au zawadi ndogo. "Wapatanishi", aina ya wapiga debe, mara nyingi walikuwa wavulana wenye umri wa kuinukia ambao walikuwa  "wakizunguka kambi" na walikuwa kama watumwa wao, ambao waliishia kufahamu lugha yao, anaelezea mkalimani wa zamani wa MONUSCO, ambaye hakutaka atajwe jina.

'Nakosa jibu'

“Sina mume, wanaume hawanitaki tena, kwa sababu nilizaa na mmoja wa wanajeshi wa kikosi cha MONUSCO, raia wa Afrika Kusini,” anaeleza Masika, mwenye umri wa miaka 29 leo. "Alikuwa kijana mzuri, jitu..." Alikuwa na umri wa miaka 15 wakati huo na alikuwa akiuza karanga karibu na duka la mjomba wake, karibu na kambi ya kijeshi ya "Adi-Kivu". Askari huyo "alimsaliti kwa miezi sita", akampa "pesa kidogo". "Nilikataa, niliogopa, lakini mwishowe nilikubali ...", anasema.

Wakati Masika aligundua kuwa ni mjamzito, askai huyo kutoka Afrika Kusini "tayari alikuwa ameondoka Kongo na nambari yake ya simu  ilikuwa haipatikani tena". Alijifungua binti, Catherine, ambaye sasa ana umri wa miaka 14 na anasoma shule ya Kavumba. MONUSCO "hulipa karo ya shule na kununua vifaa. Catherine ni mweusi kama watoto wengine wa eneo hilo na ameanza kuzoea kwa urahisi". Tatizo pekee, anamnong'oneza mama yake, "ni kwamba mara nyingi huniuliza swali la baba yake yuko wapi. Na mimi ninakosa jibu..."

Sifa, 27, pia anasema "alikaribishwa" na askari wa kulinda amani wa Afrika Kusini, ambaye hajui jina lake, alipokuwa bado hajafikisha umri wa miaka 15. Alifanya kazi katika mgahawa mdogo katika uwanja wa ndege wa Kavumba alipokuwa akisoma, jambo ambalo alilazimika kuachana nalo alipopata ujauzito. Binti yake, Grace, "hasomi". Sifa hakuchukua hatua zinazohitajika kwa wakati, "Sikuwekwa kwenye orodha ya walengwa", anajuta.

"Tulikuwa na ugumu wa kuandaa faili, kwa sababu mara nyingi wanawake hawa hawana utambulisho wa kweli wa baba wa watoto wao", anabainisha. Vipimo vya DNA kwa hivyo haziwezekani au ni ngumu sana kufanya. "Lakini tulikusanya shuhuda, kutoka kwa wasaidizi, kutoka kwa machifu wa kijiji...", anaongeza "Maman Zawadi".

Monusco hulipa "ada na vifaa vya shule", huku akina mama wakijifunza ufundi, kama vile kutengeneza vikapu au kushona, "kwa ajili ya kuwaunganisha tena kijamii". Wengine hupokea mbuzi "kwa ufugaji mdogo", anaelezea.

Inapoulizwa, MONUSCO inasema "kuhakikisha kwamba madai yote ya utumiaji na unyanyasaji wa kingono" yanayolenga walinda amani "yanashughulikiwa haraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.