DR Congo yaijibu Rwanda kutokana na kauli yake kuhusu wakimbizi
Licha ya serikali ya Kigali kuweka wazi msimamo wake kuhusu kuendelea kuwapokea wakimbizi kutoka kwa majirani zake, serikali ya Kinshasa na yenyewe imejibu na kusema kuwa imegundua ujanja wake wa kutaka kuishinikiza Jumuia ya kimataifa kulipa gharama za kila mkimbizi kutoka DRC aliyeko huko Rwanda, kama ambavyo serikali yake ilikubaliana na Uingereza kuhusu wakimbizi waliopelekwa nchini mwake.
Imechapishwa:
Cheza - 00:50
Patrick Muyaya ni msemaji wa serikali ya Kinshasa.
“Hadi Novemba mwaka wa 2022 idadi tulioipata inaonyesha kwamba wakimbizi elfu 77 kutoka Congo wapo nchini Rwanda na wamekuwa wakishawishiwa na serikali ya Rwanda wengi wao kwa bahati mbaya wamekuwa wakitumika kisiasa.”Ameeleza Patrick Muyaya
Kwa muda sasa Kinshasa imeendelea kuituhumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 wanaoyumbisha usalama Mashariki ya DRC madai ambayo Kigali imeendelea kukana.