Pata taarifa kuu
DRC- RWANDA- USALAMA

Kigali yatoa ufafanuzi kuhusu kauli ya rais Kagame juu ya swala la wakimbizi

Siku moja baada ya rais wa Rwanda Paul Kagame kuelezea kuwa nchi yake haitaendelea kulaumiwa kutokana na matatizo ya kiusalama yanayoikumba nchi jirani ya DRC na kwamba haitakubali kuwapokea wakimbizi zaidi kutoka Nchi hiyo, naibu msemaji wa serikali ya Kigali Alain Mukura-linda ametoa Ufafanuzi, baada ya kauli yake kutafsiriwa vibaya na wadau.

Rais Paul Kagame wa Rwanda na  Félix Tshisekedi wa DRC
Rais Paul Kagame wa Rwanda na Félix Tshisekedi wa DRC © Jorge Nsimba AFP montage RFI
Matangazo ya kibiashara

“Nadhani kwamba watu walishangaa na namna ambavyo rais alitumia maneno makali sababu inabidii kumwajibisha kila mtu.” Amefafanua Alain Mukuralinda.

Rwanda imekuwa ikikana madai ya jirani yake DRC kuwa inawaunga mkono waasi wa M23 wanaowashambulia raia katika eneo la mashariki ya DR Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.