Pata taarifa kuu
UGAIDI-HAKI

Kenya: Marekani yamsaka 'mhusika mkuu' wa shambulio la 2019

Marekani imetangaza siku ya Alhamisi kuwa imetenga hadi dola milioni 10 kwa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa mtu anayenatajwa kama 'musika mkuu wa kigaidi' wa shambulio dhidi ya hoteli moja nchini Kenya iliyosababisha vifo vya takriban watu 21 akiwemo Mmarekani mmoja mwaka 2019.

Mmoja wa watu waliojeruhiwa akifikishwa katika hospitali ya Garissa mnamo Novemba 4, 2012.
Mmoja wa watu waliojeruhiwa akifikishwa katika hospitali ya Garissa mnamo Novemba 4, 2012. AFP PHOTO / STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Marekani inamsaka Mohamoud Abdi Aden, ambaye inamtaja kama kiongozi wa kundi la Kiislamu la Al Shabab lenye makao yake nchini Somalia ambaye aliendesha mashambulizi kadhaa ya umwagaji damu katika nchi jirani ya Kenya.

Al Shabab, kundi lenye mafungamano na Al-Qaeda, lilidai kuhusika na shambulio la Januari 15, 2019 katika hoteli ya DusitD2 katika mji mkuu Nairobi, katika shambulio lililoendeshwa kwa takriban saa ishirini. Takriban watu 21 waliuawa, akiwemo raia wa Marekani, na wengine wengi kujeruhiwa.

Mamlaka ya Kenya ilisema wakati huo kwamba washambuliaji wote waliuawa. "Mohamoud Abdi Aden, kiongozi wa Al Shabab, alikuwa sehemu ya kundi lililopanga mashambulizi kwenye hoteli ya DusitD2," Balozi wa Marekani nchini Kenya Meg Whitman amewaambia waandishi wa habari mjini Nairobi.

Amesema Marekani imetenga zawadi ya hadi dola milioni 10 kwa habari zitakazowezesha kukamatwa kwa mtu huyo, aliyetajwa kama raia wa Kenya, na wengine waliohusika katika shambulio dhidi ya hoteli hiyo.

Mkuu wa Kurugenzi ya Uchunguzi wa Makosa ya Jinai nchini Kenya, Amin Mohamed Ibrahim, alimtaja Aden kuwa "mhusika mkuu wa kigaidi" wa shambulio hilo. Kundi la Al Shabab limemefanya mashambulizi kadhaa nchini Kenya tangu nchi hiyo ilipotuma jeshi lake nchini Somalia mwezi Oktoba 2011 kupigana dhidi ya kundi hilo la Kiislamu lenye itikadi kali.

Mnamo mwaka wa 2013, Al-Shabab walishambulia kituo cha biashara jijini Nairobi wakati wa uvamizi uliodumu siku nne, na kuua watu 67. Mnamo 2015, shambulio katika Chuo Kikuu cha Garissa mashariki mwa Kenya liliua watu 148, karibu wote walikuwa wanafunzi. Wengi wao walipigwa risasi baada ya kutambuliwa kuwa Wakristo.

Lilikuwa shambulio la umwagaji damu zaidi katika historia ya Kenya, baada ya shambulio la Al-Qaeda katika ubalozi wa Marekani mjini Nairobi mwaka 1998 na kuua watu 213.

Kundi la Al Shabab, linaloshirikiana na Al-Qaeda, limekuwa likipigana na serikali ya shirikisho inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa tangu 2007. Linachukuliwa kuwa kundi la kigaidi na Washington tangu 2008.

Mwezi Novemba, Marekani ilitangaza kuwa inatenga hadi dola milioni 10 kwa taarifa zitakazowezesha kutambuliwa kwa viongozi watatu wa Kiislamu wenye itikadi kali wa kundi la Al Shabab nchini Somalia, Ahmed Diriye, Mahad Karate na Jehad Mostafa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.