Pata taarifa kuu
KENYA-USALAMA

Kenya: Sita wafariki katika mlipuko dhidi ya basi dogo kwenye mpaka wa Somalia

Watu sita wmeuawa na saba kujeruhiwa Jumatatu wiki hii wakati kifaa cha kulipuka kilipolipuka wakati basi dogo lilipopita kaskazini mashariki mwa Kenya karibu na mpaka wa Somalia, msemaji wa polisi ya Kenya amesema.

Mji wa Mandera unapatikana Kaskazini mwa Kenya kwenye mpaka na Somalia na Ethiopia.
Mji wa Mandera unapatikana Kaskazini mwa Kenya kwenye mpaka na Somalia na Ethiopia. Google Maps
Matangazo ya kibiashara

"Kulitokea tukio baya asubuhi ya leo ambapo watu sita waliuawa katika shambulio kwenye gari," msemaji wa polisi  Bruno Shioso amesema, akiongeza kuwa shambulio hilo lilitokea saa 7:30 asubuhi (04:30 GMT).

Watu wengine saba walijeruhiwa, ameongeza alipohojiwa na shirika la habarila AFP.

Gari hilo lenye viti 14 lilikanyaga kilipuzi na kisha kufyatumliwa risasi na maguruneti, ripoti ya polisi imesema, ikionyesha kuwa shambulio hilo lilitokea takriban kilomita nane kutoka mji wa Mandera.

"Doria kutoka Kitengo kitengo maalum cha polisi ya Kenya, karibu na eneo hilo iliingilia kati na kuwakabili washambuliaji ambao walikimbia kuelekea mpaka wa Somalia", inaongeza ripoti hiyo.

Eneo la Mandera nchini Kenya linaendekea kukumbwa na mashambulizi kwenye mpaka wa Somalia, ambapo kundi la Kiislam la Somalia la Al Shabab linadhibiti maeneo makubwa ya mashambani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.