Washington yatenga dola Milioni 10 kwa atakayesaidia kukamatwa kwa Maalim Ayman
Marekani imeahidi kutoa zawadi ya Dola milioni 10 , kwa yeyote ,atakayesaidia kukamatwa kwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Shabab,Maalim Ayman , anayetuhumiwa kuongoza shambulio katika kambi yake eneo la Manda ,Pwani ya Kenya, lilosababishwa vifo vya raia wake watatu pamoja na wanajeshi kadhaa wa Kenya.
Imechapishwa:
Miaka miwili tangu shambulio hilo kwenye kambi ya Manda , inayokaliwa na wanajeshi wa Marekani êneo la Pwani ya Kenya, Marekani haijasahau tukio hilo na sasa inamsaka kiongozi wa kundi hilo.
Shambulio hilo la Januari 5 mwaka 2020 ,lilowalenga wanajeshi wa Marekani nchini Kenya lilotokelezwa kutumia roketi.
Maalim Ayman ameendelea kushtumiwa kwa kupanga mashambulio ya kigaidi nchini Kenya na Somalia kwa kipindi cha miaka kadhaa sasa.
Hadi sasa ,Marekani ,imelipa kiasi cha dola milioni 250 kwa watu 125 waliotoa ushirikiano wa kupatikana ,magaidi wanaotafutwa.