Pata taarifa kuu
USALAMA-UGAIDI

Watu 19 wauawa katika mashambulizi mawili katikati mwa Somalia

Watu 19 wameuawa katikati mwa Somalia siku ya Jumatano katika shambulio la bomu lililotegwa kwenye magari lililodaiwa na wanamgambo wenye itikadi kali wa Al-Shabab, kamanda wa wanamgambo wa eneo hilo ameliambia shirika la habari la AFP.

Mashambulizi haya yametekelezwa asubuhi huko Mahas, moja ya maeneo ya jimbo la Hiran ambapo mashambulizi makubwa dhidi ya Al Shabab yalianza miezi kadhaa iliyopita yakiongozwa na wanamgambo wa koo mbalimbali na jeshi la Somalia.
Mashambulizi haya yametekelezwa asubuhi huko Mahas, moja ya maeneo ya jimbo la Hiran ambapo mashambulizi makubwa dhidi ya Al Shabab yalianza miezi kadhaa iliyopita yakiongozwa na wanamgambo wa koo mbalimbali na jeshi la Somalia. Ilyas Hamed / AMISOM / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi haya yametekelezwa asubuhi huko Mahas, moja ya maeneo ya jimbo la Hiran ambapo mashambulizi makubwa dhidi ya Al Shabab yalianza miezi kadhaa iliyopita yakiongozwa na wanamgambo wa koo mbalimbali na jeshi la Somalia. Mashambulizi haya mapya yanaonyesha kuwa waasi, ambao wamepoteza udhibiti katika eneo hili, wanaendelea kuwa na uwezo wa kufanya mashambulizi mabaya.

"Watu kumi na tisa, wakiwemo askari wa vikosi vya usalama na raia, wameuawa katika milipuko hiyo. Magaidi (Al Shabab) wamelipua magari mawili karibu na kambi ya kijeshi huko Mahas", yapata kilomita 300 kutoka mji mkuu Mogadishu, amesema Mohamed Moalim Adan, kamanda wa wanamgambo wa eneo hilo walioshirikiana na mamlaka. Idadi ya hapo awali iliripoti vifo tisa.

"Takriban watu ishirini wameuawa katika milipuko hii miwili, wengi wao wakiwa raia, lakini mashambulizi kama hayo kamwe hayatazuia juhudi zetu za kuwaondoa," kiongozi wa ukoo wa eneo hilo Abdikarim Hassan ameliambia shirika la habari la AFP. Shahidi, Adan Hassan, amesema "aliona maiti za raia tisa, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto. Lilikuwa shambulio la kutisha", amebaini.

Kulingana na kiongozi mwingine wa ukoo, Mohamud Suleyman, takriban watu 50 pia walijeruhiwa katika milipuko hiyo. Al-Shabab wamedai kuhusika na shambulio hilo, wakidai kulenga "kambi za kijeshi".

Kundi hili linaloshirikiana na Al-Qaeda, limekuwa likipigana na serikali ya shirikisho inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa tangu 2007. Lilitimuliwa nje ya miji mikuu ya nchi mwaka 2011-2012, lakini limebaki imara katika maeneo makubwa ya vijijini.

"Vita kamili"

Mapema mwezi Julai, koo mbalimbali katika jimbo la Hiran ziliasi dhidi ya waasi wa Kiislamu. Serikali ya Hassan Cheikh Mohamoud, ambayo imeahidi "vita kamili" dhidi ya kundi la Kiislamu, ilituma jeshi mnamo Septemba - ikiwa ni pamoja na vikosi maalum - kusaidia wanamgambo hawa wanaojulikana kama 'Macawisley'.

Mashambulizi haya, yakiungwa mkono na jeshi la Umoja wa Afrika nchini Somalia (Atmis) na mashambulizi ya anga ya Marekani, yalifanya iwezekane kuteka tena maeneo makubwa katika majimbo mawili katikati mwa nchi, Hirshabelle - ambapo jimbo la Hiran linapatikana - na Galmudug.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.