Pata taarifa kuu

Pembe ya Afrika: Watoto milioni 20 wako katika dharura ya chakula, yaonya UNICEF

Zaidi ya watoto milioni 20 wako katika hatari ya njaa, kiu na magonjwa nchini Ethiopia, Kenya na Somalia, kulingana na ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto, UNICEF, iliyotolewa Alhamisi (Desemba 22). Mabadiliko ya Tabia nchi, migogoro, mfumuko wa bei na uhaba wa nafaka vinaathiri pakubwa eneo la Pembe ya Afrika.

Kutokana na uhaba wa maji, familia kadhaa nchini Ethiopia, Kenya na Somalia zinakabiliwa na hali mbaya.
Kutokana na uhaba wa maji, familia kadhaa nchini Ethiopia, Kenya na Somalia zinakabiliwa na hali mbaya. © AP/Jerome Delay
Matangazo ya kibiashara

Walikuwa milioni kumi mwezi Julai mwaka huu. Sasa ni milioni 20.2. Kwa hivyo, zaidi ya mara mbili, licha ya juhudi za mashirika ya kibinadamu. "Wakati juhudi za pamoja za kuharakishwa zimepunguza baadhi ya athari mbaya zaidi za kile kilichohofiwa," amebaini Naibu Mkurugenzi wa UNICEF katika Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Lieke van de Wiel, watoto katika Pembe ya Afrika bado wanakabiliwa na ukame mbaya zaidi katika zaidi ya vizazi viwili. 

Wito wa michango kutoka UNICEF

Takriban watoto milioni mbili nchini Ethiopia, Kenya na Somalia wanahitaji matibabu ya haraka kutokana na utapiamlo uliokithiri, "njaa mbaya zaidi", linasema shirika la Umoja wa Mataifa. Kwa kuzingatia uhaba wa maji, familia zinakabiliwa na hali mbaya. Na hii huongeza shinikizo kwa watoto, pamoja na unyanyasaji, kazi ya kulazimishwa au ndoa, au ukeketaji, unyanyasaji wa kijinsia au usio wa kijinsia, hasa wasichana wadogo.

UNICEF ​​​​inatoa wito wa michango: dola Milioni 759 ili kukidhi mahitaji katika mwaka 2023. Dola milioni 690 za ziada zinaweza kuwezesha watoto na familia zao kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.