Pata taarifa kuu

Ukosefu wa mvua wasababisha wau kukubwa na njaa Pembe ya Afrika

Mamilioni ya watu katika nchi za pembe ya Afrika, za Kenya, Somalia na Ethiopia, wanakabiliwa baa la njaa kufuatia kutokuwa na mvua ya kutosha iliyosababisha mazao kutonawiri mashambani. 

Somalia inakabiliwa na ukame unaoendelea.
Somalia inakabiliwa na ukame unaoendelea. © AP Photo/Elias Meseret
Matangazo ya kibiashara

Watalaam wa hali ya hewa wanasema kwa misimu minne sasa, hali imeendelea kuwa mbaya na hali hii huenda ikashuhudiwa tena kati ya mwezi Oktoba na Novemba, miezi ambayo inatarajiwa kushuhudia uhaba wa mvua. 

Aidha, wanasema hali ya mabadiliko ya hali ya hewa inayoshuhudiwa kwa sasa, haijawahi kuonekana kwa miaka 40 sasa, hasa katika kipindi hiki cha kati ya mlwezi Machi na Mei ambacho hufahamika kuwa kipindi cha mvua nyingi, lakini kuna ukame. 

Mbali na ukame kusababisha uharibifu wa mazao, mifungo zaidi ya Milioni tatu, ikifariki katika baadhi ya maeneo nchini Kenya na Ethiopia na  watu wakilazimika kuyahama makwao kwenda kutafuta chakula na maji. 

Shirika la mpango wa chakula linaonya kuwa, idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa huenda ikaonhezeka kutoka Milioni 16.7 hadi Milioni 20 ifikapo mwezi Septemba. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.