Pata taarifa kuu
Penya ya Africa - Baa la njaa

UN yataka Kenya, Somalia na Ethiopîa kusaidiwa kukabili ukame

Umoja wa Mataifa, umetoa mwito wa dharura wa kupatikana fedha ili kusaidia mataifa ya pembe ya Afrika, ambayo kwa miezi yameshuhudia hali ya ukame inayotishia kuwa mbaya zaidi.

Baa la njaa laathiri Pembe ya Africa
Baa la njaa laathiri Pembe ya Africa Reuters/ Thomas Mukoya/
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mkuu wa tume ya misaada ya umoja wa Mataifa, Martin Griffiths, muda wa kupoteza haupo tena na kwamba fedha hizo zinahitajika kwa haraka kuokoa maisha ya watu.

UN inasema eneo la Pembe ya Afrika linashuhudia ukame mbaya zaidi kuwahikutokea, ambapo watu milioni 15 katika nchi za Ethiopia, Kenya na Somalia wanakabiliwa na baa la njaa.

Haya yanajiri wakati huu viongozi wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakiwataka raia kutunza chakula cha kutosha.

Mwishoni mwa mwaka jana, UN ilizindua kampeni ya kupata dola za Marekani bilioni 41 kusaidia watu milioni 274 wanaohitaji msaada na ulinzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.