Pata taarifa kuu
SOMALIA- USALAMA

Milipuko Somalia: Al Shabab wamekiri kuhusika

Watu 19 wameuawa kwenye mashambulio mawili ya bomu, katikati ya nchi ya Somalia, mashambulio ambayo magaidi wa Al Shabab wamekiri kutekeleza, na kudai pia kushambulia kambi za jeshi katika miji ya miji ya Mahasa na Dadan Ad.

Wapiganaji wa Al Shabab
Wapiganaji wa Al Shabab AP - Farah Abdi Warsameh
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa kiongozi wa kundi lenye silaha  linaloshirikiana na serikali kupambana na magaidi hao katika eneo hilo la Mahasa ,Mohammed Moalim Adan ,waliopoteza maisha ni wanajeshi pamoja na raia, huku wengine 52 wakijeruhiwa.

Kundi hilo limesema mashambulio hayo ya jana  yalihusisha ;magari mawili yaliyokuwa na vilipuzi ,yaliyolipuliwa katika mji wa Mahas, iliyokuwa ngome ya Al Shabab kabla ya kutimuliwa mwaka uliopita.

Aidha, Kamanda wa polisi êneo hilo Osman Nur ,amesema , magaidi hao walikuwa wameamua kuwalenga raia wasio na hatia baada ya kuonekana kuzidiwa nguvu kwenye operesheni ya vikosi vya serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.