Pata taarifa kuu

Raia wa DRC watiwa wasiwasi na hatua ya rais Kagame

Hatua ya rais wa Rwanda, Paul Kagame kuwa haitakuwa tayari kuwapokea wakimbizi kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wanaokimbia machafuko ya mara kwa mara, imezua wasiwasi kuhusu usalama wa raia wa DRC wanaotafuta usalama. 

Kituo cha mpakani kati ya DRC na Rwanda katika wilaya ya Rubavu.
Kituo cha mpakani kati ya DRC na Rwanda katika wilaya ya Rubavu. AFP/ALAIN WANDIMOYI
Matangazo ya kibiashara

Kagame ametoa kauli hii siku ya Jumatatu, akieleza kughadhabishwa kwake na madai ya serikali ya DRC na mataifa ya kigeni kuwaunga mkono waasi wa M 23, wakati inawapa msaada raia wake. 

"Hatuwezi kuzungumza nao kwa sababu ni magaidi hiyo ndiyo imekuwa kauli ya DRC ikisema kwamba haiwezi kuzungumza na M23 kwa sababu ni magaidi.” alisema rais Kagame.

Kwa miaka kadhaa sasa, Rwanda imekuwa ikiwapa hifadhi wakimbizi zaidi ya Elfu themanini, wengi wao wakiwa kutoka jamii ya Wanyamulenge waliokimbia nchini DRC kwa sababu ya utovu wa usalama.

Haya yanajiri wakati huu nchi ya DRC, Marekani na mataifa kadhaa ya Ulaya, yakiutuhumu utawala wa Kigali kwa kuwasaidia waasi wa M23, tuhuma ambazo rais Kagame amezikanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.