Pata taarifa kuu
DRC-UGANDA- USALAMA

Uganda yapeleka wanajeshi katika mpaka na DR Congo kuzia M23

Serikali ya Uganda, imepeleka wanajeshi wake katika eneo la mpaka wa nchi hiyo na DRC katika wilaya ya Kanungu, ambako waasi wa M23 wameendelea kuingia katika mji wa Ishasha, baada ya kuondoKa Kibumba.

Waasi wa M23
Waasi wa M23 AFP - GLODY MURHABAZI
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa lutein kanali Robert Nahamya, wanajeshi hao walitumwa tangu siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita, lengo likiwa ni kutoa usalama kwa raia wake wanaoishi kwenye eneo hilo la mpaka.

Taarifa kutoka DRC zinasema waasi wa M23 wameendelea kuchukua vijiji muhimu na maeneo ya masoko karibu kilometa 20 na mpaka wa mji wa Ishasha.

Kwa mujibu wa jeshi la DRC na ripoti za usalama za Umoja wa Mataifa, waasi wa M23 wameendelea kutuma ujumbe unaokinzana na kauli zao za juma lililopita, kuwa wataondoka bila masharti katika miji waliyokuwa wanaishikilia.

Hata hivyo licha ya agizo la vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutaka waasi hao kuachia miji wanayoshikilia chini ya makubaliano ya Nairobi na Luanda, wapiganaji wake wameripotiwa kushambulia raia katika miji wanakopita.

Mapigano kati ya wanajeshi wa Serikali ya DRC na waasi wa M23, yalizuka mwezi Machi mwaka uliopita, na kulazimisha watu zaidi ya elfu 70 kukimbilia nchini Uganda kuomba hifadhi, huku nchi ya Rwanda ikituhumiwa kuwasaidia waasi hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.