Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Maelfu yatoroka makazi yao kufuatia kuzuka kwa mapigano ya kikabila Sudan Kusini

Nchini Sudan Kusini, kunashuhudiwa mapigano mapya yaliyoanza Septemba 23, kati ya makabila mawili yanayoishi katika majimbo yenye utajiri wa mafuta ya Upper Nile na Unity. 

Katika Kambi ya Gumbo, Sudan Kusini, wanawake waliokimbia makazi yao wanatayarisha chakula kutoka kwa majani yaliyokusanywa karibu na kambi yao.
Katika Kambi ya Gumbo, Sudan Kusini, wanawake waliokimbia makazi yao wanatayarisha chakula kutoka kwa majani yaliyokusanywa karibu na kambi yao. © RFI/Florence Miettaux
Matangazo ya kibiashara

Mapigano haya yaliyoanza yamekemewa vikali na Nicholas Haysom, mwakilishi maalum wa Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini. Aliwahutubia waandishi wa habari katika afisi za UNMISS siku ya Alhamisi. 

Tangu Septemba 20  mapigano kati ya watu kutoka kabila la Twich na Ngok Dinka, yamesababisha mlipuko mpya wa wakimbizi. Mapigano mapya kikabila  yanaendelea machafuko. Mapigano hayo yamesababisha maelfu ya watu kukosa makao katika majimbo ya upper Nile na Unity. Watu elfu-kumi-na-nne hawana makao na sasa tuemewapa mahali pa kuishi ambapo wanalindwa na vikosi vyetu vya usalama katika mji wa Malakal, mji mkuu wa jimbo la Upper Nile. UNMISS inajaribu kadri inavyoweza kutayarisha mahali watu wanaotoka kwenye sehemu za mapigano makali wataishi na kulindwa, lakini inategemea na hela tulizo nazo. Mapigano kati ya makabila mawili: Twich na Ngok Dinka, yamesababisha kuongezeka upya kwa wakimbizi katika jimbo la Abyei.

Abyei ni jimbo lenye utata kwani Sudan inadai kuwa ni sehemu ya nchi yake na Sudan Kusini inashikilia kuwa jimbo hilo liko katika nchi hiyo. Akithibitisha kuwa kweli mapigano yanaendelea, waziri wa habari Michael Makwei, alisema: 

Ninachofahamu ni kwamba kuna mapigano ya jumuiya ya makabila ama mapigano ya kikabila. Hayo ndiyo ninayofahamu kwa sasa na mapigano hayo yanakabiliwa na serikali ipasavyo. Hayo ndiyo mimi nafahamu kwa sasa. 

Tangu Sudan kusini itangazwe kuwa nchi huru duniani mwaka 2011, imekumbwa na mapigano kikabila. Mapigano hayo yanatokana na zogo kuhusu linalohusiana na ardhi ya malisho ya mifugo na kabila lenye haki ya kutumia maji. Hali kadhalika mapigano yamesababishwa na makundi yanayopigana kumiliki sehemu za kuzalisha mafuta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.