Pata taarifa kuu
HAKI-UFISADI

Waziri wa Utamaduni na Vijana Edouard Bamporiki aombwa kufungwa jela kwa kosa la ufisadi

Viongozi wa Mashtaka nchini Rwanda, wanataka kufungwa jela kwa aliyekuwa waziri wa Utamaduni na Vijana Edouard Bamporiki, ambaye ameshtakiwa kwa kosa la ufisadi na kutumia mamlaka yake kwa masilahi binafsi. 

Paul Kagame, Rais wa Rwanda.
Paul Kagame, Rais wa Rwanda. REUTERS - JEAN BIZIMANA
Matangazo ya kibiashara

 

Mbali na kifungo, viongozi wa mashtaka wametaka Bamporiki pia kutozwa faini ya Faranga za Rwanda Milioni 200 sawa na Dola Laki moja na Elfu themanini na nane. 

Waziri huyo wa zamani mwenye umri wa mika 39, amekiri mashtaka dhidi yake katika Mahakama ya Nyarugenge, jijini Kigali. 

Mbele ya Mahakama, Bamporiki, ameomba radhi na kujitetea kuwa alilazimika kuhusika na kosa hilo ili kumsaidia rafiki yake ambaye kampuni yake ya bia ilikuwa imesimamishwa. 

Kabla ya kushtakiwa, Rais Paul Kagame alimsimamisha kazi mwezi Mei na kuagiza achunguzwe kwa madai ya ufisadi, na toka kipindi hicho amekuwa katika kifungo cha nyumbani. 

Baada ya hatua hiyo, alitumia ukurasa wake wa Twitter na kukiri kuwa alipokea rushwa na kumwomba radhi rais Kagame. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.