Pata taarifa kuu
DRC - RWANDA

Angola : Viongozi wa Rwanda na DRC wakutana tena

Viongozi wa Rwanda na DRC, wamekutana tena juma hili mjini Luanda, Angola, ambapo walijadiliana namna bora ya kumaliza mvutano ulioko baina yao kuhusu makundi ya waasi yanayofanya shughuli zao kwenye êneo la mashariki mwa DRC.

Marais wa Rwanda Paul Kagame, João Lourenço wa Angola na Félix Tshisekedi  wakati wa mkutano wao  mjini Luanda, Julai 6, 2022, kuhusu mvutano mashariki mwa DRC.
Marais wa Rwanda Paul Kagame, João Lourenço wa Angola na Félix Tshisekedi wakati wa mkutano wao mjini Luanda, Julai 6, 2022, kuhusu mvutano mashariki mwa DRC. AFP - JORGE NSIMBA
Matangazo ya kibiashara

Katika mazungumzo yaliyoanza Jumatano na kutamatika hapo jana, viongozi wa nchi zote mbili wamekubaliana kuhusu waasi wa M23 kuondoka katika maeneo wanayoyashikilia.

Viongozi hao pia wametaka kuharakishwa kupelekwa kwa jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo nchi ya Rwanda haitashiriki lakini wakakubaliana kuhusu kupigana na makundi yote ikiwemo FDLR.

Taarifa ya pamoja ya pande hizo mbili, pia imeongeza kuwa kamati maalumu iundwe harala ili kuchunguza madai yaliyotolewa na nchi hizo pamoja na vurugu za kwenye mipaka, huku pia wakikubali kufanya kazi kwa pamoja kwa mustakabali wa amani.

Nchi hizi mbili pia zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika maeneo ya biashara na kijamii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.