Pata taarifa kuu
Rwanda - Siasa

Rwanda : Kagame kuwania urais mwaka 2024

Rais wa Rwanda Paul Kagame, amesema atawania tena urais katika uchaguzi wa mwaka 2024.

Paul Kagame, siku chache kabla ya uchaguzi wa Agosti 2017.
Paul Kagame, siku chache kabla ya uchaguzi wa Agosti 2017. REUTERS/Jean Bizimana
Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano na runinga ya  France 24, Kagame mwenye miaka 64 amesema analenga kuwania urais kwa miaka mingine 20 ijayo na kusisitiza kuwa uchaguzi unahusu  wananchi kumchagua kiongozi wanayemtaka.

Mwaka 2015, rais Kagame alibadili katiba ya taifa hilo na sasa inamruhusu kusalia madarakani hadi mwaka 2034.

Katika uchaguzi uliopita Kagame alishinda uchaguzi kwa aslimia 99, uchaguzi ambao wapinzani wake walipinga vikali matokeo.

Licha ya rais Kagame kushtumiwa kwa kukiuka haki za binadamu, ameendelea kutetea utawala wake hata katika mikutano ya kimataifa kama ile ya Jumuiya ya Madola iliofanyika mwezi Juni jijini Kigali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.