Pata taarifa kuu
Rwanda - Usalama - siasa

Rwanda : Rais Kagame aapa kulinda Rwanda

Rais wa Rwanda, Paul Kagame, amesema mzozo kati yake na DRC utaendelea kushuhudiwa ikiwa wadau husika wataendelea kupuuza ukweli kuhusu kiini cha mzozo unaoripotiwa kwa sasa, akionya kuilinda nchi yake kwa kila namna dhidi ya maadui.

Rais wa Rwanda Paul Kagame,
Rais wa Rwanda Paul Kagame, REUTERS - JEAN BIZIMANA
Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano maalumu na waandishi wahabari jijini Kigali, rais Kagame aliibua swala la wapiganaji wa FDLR ambao hivi karibuni waliripotiwa kushirikishwa na jeshi la Kongo katika vita dhidi ya waasi wa M23, rais Kagame akitaka suluhu ya amani ipatikane.

Rais Kagame pia amengumzia taarifa kuhusu uwezekano wa wanajeshi wake kutojumuishwa katika kikosi cha pamoja cha Jumuiya ya Afrika Mashariki kitakachoundwa hivi karibuni, akisema Rwanda haina tatizo iwapo hilo halitashirikishwa katika kikosi cha pamoja cha jumuiya ya Africa mashariki.

Aidha rais kagame amesema mzozo wa mashariki mwa DRC, hauwezi suluhishwa kupitia vita, akipendekeza suluhu la kisiasa kutumika.

Kwa majuma kadhaa sasa, Serikali ya DRC imeendelea kusisitiza kuwa uasi unaofanywa na wapiganaji wa M23, umetokana na kundi hilo kupata usaidizi kutoka Rwanda, Kinshasa ikidai hata wanajeshi wa RDF waliingia kwenye ardhi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.