Pata taarifa kuu
Rwanda Usalama

Rwanda: Mshukiwa wa mauwaji ya kimbari athibitishwa kufariki

Kamati ya umoja wa mataifa, imetangaza kifo cha mmoja wa washukiwa wakuu wa mauwaji ya kimbari, nchini Rwanda, Phénéas Munyarugarama, ambaye amekuwa akisakwa kwa muda.

Phénéas Munyarugarama
Phénéas Munyarugarama © achieve
Matangazo ya kibiashara

Kamati hiyo ya umoja wa mataifa inayoshughulikia maswala ya uhalifu, imesema Pheneas, ambaye alikuwa miongoni mwa washukiwa wakuu wa watano wa mauwaji hayo ya kimbari, alifariki mwaka 2002 akiwa mashariki mwa DRC.

Kamati hiyo imeafikia kutoa ripoti hiyo kutokana na uchuguzi wa kina, kwamba Pheneas, alifariki kifo cha kawaida, tarehe 28 mwezi wa pili mwaka 2002.

Pheneas ambaye alikuwa kamanda wa jeshi la Rwanda, alikuwa anahushwa na mashtaka nane ya uhalifu wa kivita.

Kiongozi wa mashtaka wa kamati hiyo, Serge Brammertz, amesema wanatumai ripoti yao italeta matumai kwa raia wa Rwanda hasa wanaoishi eneo la Bugesera ambako, Pheneas alitekeleza uhalifu huo.

Taarifa hii inajiri juma moja baada ya kamati hiyo kuthibitisha kifo cha mshukiwa mingine wa mauwaji hayo ya kimbari Protais Mpiranya.

Zaidi ya raia 800,000 waliuawa nchini Rwanda, kwa kipindi cha siku 100 mwaka 1994.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.