Pata taarifa kuu

Rwanda: Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari Mpiranya amedhitishwa kufariki

Moja ya watu wa mwisho waliokuwa watuhumiwa wakuu wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, Protais Mpiranya, sasa imethibitishwa alifariki nchini Zimbabwe tangu mwaka 2006.

Picha iliyochapishwa na umoja wa mataifa ikimuonyesha Protais Mpiranya,
Picha iliyochapishwa na umoja wa mataifa ikimuonyesha Protais Mpiranya, AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa waendesha mashtaka wa umoja wa Mataifa, Mpiranya alikuwa ameshtakiwa kwa makosa ya mauaji, uhalifu wa kivita na dhumma dhidi ya binadamu, ambapo wakati huo alikuwa kiongozi wa walinzi wa rais.

Waendesha mastaka hao ambao wametumia muda wa karibu miongo miwili kumsaka, baada ya kukutwa na hatua na mahakama ya umoja wa Mataifa mwaka 2000, imefahamika alifariki miaka 16 iliyopita kutokana na ugonjwa wa kifua kikuu.

Ofisi ya mahakama hiyo ya mjini the Hague, imesema Mpiranya alikuwa mmoja ya watuhumiwa wakuu waliokutwa na hatia katika mahakama ya ICTR na anatajwa kuhusika pakubwa na mauaji ya mwaka 1994 dhidi ya Watusi.

Alikuwa mtuhumiwa mkuu pekee aliyesalia kukamatwa baada ya miaka miwili iliyopita, mtuhumiwa mwingine Felicien Kabuga, kukamatwa nchini Ufaransa.

Mpiranya anatajwa kuhusika na mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu Agathe Uwilingiyimana, wanajeshi 10 wa Ubelgiji waliokuwa wanamlinda pamoja na wanasiasa wengine mashuhuri nchini Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.