Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-USALAMA

Pande mbili za viongozi wa Sudani Kusini zashtumiana kuvunja mkataba wa amani

Shirika la Chakula Duniani, WFP, limewaondoa wafanyakazi wao mia moja na arobaini, kutoka  Kaunti ya Ler, iliyoko kwenye  jimbo la Unity, kaskazini-magharibi mwa Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, ambako mapigano makali yanaendelea kati ya vikosi tiifu kwa Rais Salva Kiir na wanajeshi wanaomtii naibu wake Riek Machar.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (kushoto) na makamu wake, kiongozi wa zamani wa waasi Riek Machar (kulia) mjini Juba Februari 20, 2020 wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (kushoto) na makamu wake, kiongozi wa zamani wa waasi Riek Machar (kulia) mjini Juba Februari 20, 2020 wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari. REUTERS/Jok Solomun
Matangazo ya kibiashara

Kuondolewa kwa wafanyakazi hao kulifuatiwa na kupelekwa Ler, wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kutoka Ghana, kulinda raia. 

Mwakilishi wa shirika la Chakula Duniani, nchini Sudan Kusini, Mathew Hollingworth, anasema kuwa mapigano hayo yamesababisha vifo vya watu thelathini na wengine zaidi ya elfu ishirini na tano wamekosa makaazi, katika Kaunti ya Ler.

Inatia uonga. Kile tulichoona kikitendeka kwa watu kina sikitisha. Watu wameuawa, kujeruhiwa, wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada wameondolewa huko kutokana na mapigano yanayoendelea. Sasa kuna watu wengi ambao wametokomea msituni kujificha kuokoa maisha yao. jengo ya shirika la Chakula Duniani limebomolewa na kila kitu kuibiwa. Haya yanatendeka kwa mwaka ambao utakuwa mgumu. Kuleta misaada ya kusaidia watu wa Sudan, kutakuwa kugumu sana kwetu. 

Hollingworth alipokuwa akizungumza, wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kutoka Ghana waliwasili katika Kaunti ya ler, kuwalinda raia. Kaunti ya Ler, ina watu wengi kuliko kaunti zote nchini Sudan kusini. 

Wanajeshi wa Umoja wa mtaifa Sudan Kusini, wanazunguka kila mahali na kushirikiana pamoja na wananchi kuhakikisha kuwa hali ni salama. « Kwa jumla hali ni mbaya. Wanajeshi wetu kutoka Ghana wako ler kulinda watu walioathirika. Wanafanya kazi pamoja na wakuu wa ler na pia kuwapa watu maji safi ya kunywa na kutoa matibabu », Umoja wa Mataifa umesema katika taarifa . 

Mapigano katika kaunti ya Ler yanahusisha vikosi tiifu kwa Rais Salva Kiir na wanajeshi wanaomtii naibu wake Riek Machar. 

"Mashambulizi ya kinyama yalitekelezwa na jeshi tiifu kwa Rais Salva Kiir la SSPDF. Mashambulizi hayo yanakiuka mkataba wa kusitisha mapigano na mkataba wa amani. Mashambulizi yalianza wakati SSPDF iliposhambilia ngome yetu katika kaunti ya Ler. Mashambulizi yaliongozwa na mwanajeshi wa cheo cha kanali. Kwetu sisi mashambulizi ni mpango wa kuanza tena kwa vita, kitendo kilichoanzishwa na SSPDF " , amesema msemaji wa Riek Machar, Pok Both Balanga. 

Mapigano yanayoendelea yanakuja majuma mawili baada ya Rais Salva Kiir na naibu wake Riek Machar kusaini mkataba mpya ambao utaungansisha vikosi vyote vya kijeshi kuwa jeshi moja la taifa pakiwamo polisi. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.