Rais wa Sudan Kusini aanza kutia katika vitendo mkataba wa aman iwa 2018
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, ameunda komandi mpya ya jeshi la pamoja, inayojumuisha vikosi vya upinzani, ikiwa ni utekelezaji wa kipengele muhimu katika mkataba wa amani wa mwaka 2018.
Imechapishwa:
Hatua hii inakuja baada ya mapigano ya hivi karibuni kati ya vikosi vya Kiir na Machar, kusababisha zaidi ya watu Elfu 14 kuyakimbia makwao.
Baada ya hatua hii, wanajeshi na polisi watapata mafunzo ya pamoja ndani ya miezi miwili, kwa mujibu wa makubaliano hayo.
Kulikuwa na wasiwasi kuhusu kutokea mapigano mapya nchini Sudan Kusini, kati ya vikosi tiifu kwa Salva Kiir na Riek Machar, kila mmoja akimtuhumu mwingine kwa kukiuka mkataba wa amani.