Pata taarifa kuu
KENYA-UHABA WA MAFUTA

Kenya yamfukuza Jean-Christian Bergeron kwa tuhuma za kuficha mafuta

Serikali ya Kenya imemfukuza nchini humo, Jean-Christian Bergeron, Mkurugenzi wa Kampuni ya Ufaransa Rubis Energy kwa kumhusisha na kile kinachoelezwa ni kuficha mafuta na kusababisha uhaba wa bidhaa hiyo muhimu katika taifa hilo.

Wakenya wakiwa kwenye foleni katika kituo cha mafuta cha Nairobi.
Wakenya wakiwa kwenye foleni katika kituo cha mafuta cha Nairobi. AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa nishati nchini humo Monica Juma, ambaye amethibitisha kuondoka kwa Mkurungezi huyo, ameonya wasambazaji wa mafuta kuacha kuzuia bidhaa hiyo, huku akiwahakikishia Wakenya kuwa nchi hiyo ina mafuta ya kutosha na hali itarejea kama kawaida baada ya saa 72.

Katika hatua nyingine, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati nchini humo EPRA imeongeza bei ya mafuta.

Kuanzia saa sita usiku, Petroli itauzwa Shilingi za Kenya 144.62 ambalo ni ongezeko la Shilingi tisa. Diesel sasa itauzwa Shilingi 125.5.

Hii inaelezwa kuwa bei kubwa ya mafuta kuwahi kushuhudiwa nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.