Mwanasiasa wa Rwanda afukuzwa nchini Uganda
Uganda imesema imemfukuza nchini humo Robert Mukombozi mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda, ambaye chama chake cha Rwandan National Congress (RNC) kimepigwa marufuku.
Imechapishwa:
Hii imeonekana kama ishara ya Kampala na Kigali kuanza tena kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia ambao ulikuwa umeyumba miaka kadhaa iliyopita.
Aidha, hatua hii imekuja baada ya kuwepo kwa jitihada za kidiplomasia ambazo zimekuwa zikiongozwa na mtoto wa rais wa Uganda Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba ambaye amekuwa akizuru jijini Kigali na kukutana na rais Paul Kagame.
Hatua hii ilisababisha kufunguliwa kwa mpaka wa Gatuna, uliokuwa umefungwa.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Kainerugaba ameandika kuwa, Mukombozi amefukuzwa Uganda kwa sababu yeye ni adui wa Rwanda na Uganda , na kuchapisha picha zake akielekea kuabiri ndege kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe.
I don't like doing this, but if it saves the lives of my soldiers, I will do anything. I thank CMI, under Maj.General Birungi for this excellent operation. This enemy of Uganda and Rwanda was picked up and sent back to wherever he came from. pic.twitter.com/Z1Y2DktyqO
— Muhoozi Kainerugaba (@mkainerugaba) April 2, 2022
Mukombozi, raia wa Rwanda, alizaliwa nchini Uganda, na amewahi kuwa mwanahabari kabla ya kwenda Rwanda, lakini baada ya kutofautiana na serikali, alikimbilia nchini Australia, kwa mujibu wa Habari za Kiinteljensia za nchi hiyo.