Pata taarifa kuu
UGANDA-SIASA

Uganda: Kustaafu kwa mtoto wa Museveni jeshini kwaibua maswali mengi

Je, huko Uganda mtoto wa Rais Museveni atamrithi baba yake? Muhoozi Kainerugaba alitangaza Jumanne Machi 8 yuko tayati kustaafu jeshini wakati alikuwa mmoja wa viongozi wakuu majeshi ya Uganda. Tangazo hili limezua uvumi kuhusu kurithishwa kwa familia katika uongozi wa nchi.

Muhoozi Kainerugaba wakati wa kuapishwa kwake kama mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Uganda Januari 17, 2017.
Muhoozi Kainerugaba wakati wa kuapishwa kwake kama mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Uganda Januari 17, 2017. AFP - PETER BUSOMOKE
Matangazo ya kibiashara

"Baada ya miaka 28 ya kuhudumu katika jeshi langu tukufu, jeshi kubwa zaidi ulimwenguni, nina furaha kutangaza kustaafu". Hivi ndivyo Muhoozi Kainerugaba aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter.

Ana cheo cha jenerali na ameongoza jeshi tangu mwezi Juni 2021, baada ya kuongoza kikosi maalum. Muhoozi Kainerugaba ana umri wa miaka 48 na ametangazwa kwa miaka kadhaa sasa kama mrithi anayetarajiwa wa babake Yoweri Museveni, mamlakani huko Kampala tangu mwaka 1986.

Rais wa sasa ambaye, hata kama anapenda kuonyesha hali yake nzuri ya kimwili - alilimwona akipiga push-ups wakati wa kampeni za mwisho katika uchauzi wa urais - ana umri wa miaka 77.

Pongezi kwa Paul Kagame

Nafasi ya Muhoozi Kainerugaba jeshini, pamoja na nafasi yake ya "mshauri mkuu wa rais anayehusika na operesheni maalum", zinamfanya kuwa mgombea mkubwa wa madaraka.

Katika ukurasa wake wa Twitter, hivi majuzi alitilia mkazo sana kufunguliwa kwa mpaka na Rwanda, na alionyesha kuvutiwa kwake na Paul Kagame, ambaye alikutana naye mjini Kigali mwishoni mwa mwezi Januari. Pia alionyesha uungaji mkono wake kwa Urusi, akisema kuhusu Ukraine kwamba "Putin yuko sahihi kabisa".

Mada ya urithi ni tete nchini Uganda. Mwandishi Kakwenza Rukirabashaija hivi majuzi alilazimika kutoroka nchi baada ya matamshi ya dharau dhidi ya utawala wa Museveni, kulingana na kauli ya serikali. Hapo awali alikamatwa na kuteswa kwa kumdhihaki mtoto wa rais kwenye mitandao ya kijamii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.